Kuna mtu anajua wewe ni...

Martin BM

Member
Joined
Jul 2, 2020
Posts
16
Reaction score
22
MARA nyingi AKILI yangu huwa inafanya kazi kulingana na mtu ninaekutana nae.
Kuna mtu anajua mimi ni mjinga.

Kuna mtu anajua mimi ni mtu mwenye upeo mpana wa kufikiri.

Kuna mtu anajua mimi ni mpole harafu kuna mtu anajua mimi ni bonge la mkorofi.
Kuna mtu anajua mimi ni mcheshi harafu kuna mtu anajua mimi ni bonge la kauzu. [emoji119][emoji2217]

Je, kwa upande wako hapo kuna mtu anajua wewe ni (malizia hapo).
 
Muhimu kuliko vyote ni kwamba Mungu anakuchuliaje wewe, halafu pili wewe unajichukuliaje. Maoni ya watu wengine kuhusu wewe yasikuumize sana kwasababu wanadamu tuna LIMITED ALTRUISM. Huwezi kupendwa na wanadamu wote na pia huwezi kuchukiwa na wanadamu wote: Mtu ambaye hanilishi wala hanivishi akinipuuza au kunisifia huwaga siwazi kabisa, maana Mungu anavyoniona na mimi ninavyojiona ndiyo muhumu zaidi.
 
Wewe kama wewe, Mungu anakuonaje...?
 
Kama mtu yupo nje ya cycle yako
Je, Kuna umuhimu wa kujua anakufikiriaje maana huwa naona kama unamuuliza mtu kuhusu imaginations zake badala ya reality
 
Kama mtu yupo nje ya cycle yako
Je, Kuna umuhimu wa kujua anakufikiriaje maana huwa naona kama unamuuliza mtu kuhusu imaginations zake badala ya reality
Exactly the Point,........
 
Muonekano tu na matendo yangu yanajionesha tu nilivyo.
 
Anajua anachokijua yeye sijaingia kwenye akili yake kwa hiyo asiniumize kichwa kutaka nijue ananichukuliaje.

Anichukulie kivyovyote ajuavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…