What's the use...
Hamna BAN hapa wala babu yake na ban, unamwadhibu mwanamke ili iweje kwamba ukimuadhibu ndio ataacha??? Lazima ujiulize kwanza sababu za huyo mwanaume kumsamehe huyo mwanamke mara tatu.
So unamshauri aendelee/aombe/amuombee mke wake tu?
Asimuache kwa sasa? Maana ana mpango wa kumuacha ila hajui aanzie wapi, kuiambia jamii yake anamuacha mke wake,
kisa kamfumania, anamuonea huruma mkewe huyo, manake ni aibu kubwa ujue. Unarudishwa kwenu na na ushahidi mzito wa kufumaniwa,
Dah, kipenzi cha moyo wake, mama wa watoto wake, mtu aliye/anayempenda kwa dhati.
Inauma Aisee!!!
Nnayo maswali mengi nataka kumuuliza huyo jamaa yako.
- Huyo jamaa yako anamtosheleza mdada kwa namna zote ukiacha mahitaji ya chakula, nguo, etc.
- Mdada aliwahi kumfumania jamaa hata mara moja?
Hivi kama mume wako anakupenda na kukujali kwa kila kitu kisha huko nyuma hukuwa mwaminifu na ukakubali na akakusamehe. ukarudia tena mara 2 au tatu na akakuonya na kukusamehe. Je akikukukuta tena una mahusiano nje ya ndoa akufanye nini?
Mbarikiwe sana.
Nimesahau kuanza na Salamu, ila nina Imani nyote hamjambo. Karibuni kikombe cha chai hapa. Haya tunaomba msaada wa mawazo wapendwa.
...mnh, Ok...kumbe tayari ana mpango wa kumuacha ila hajui aanzie wapi?
Aanzie hapo hapo bana. Talaka, kisha ampe haki yake vile walivyochuma pamoja.
...thubutu! unadhani kuna mwanaume atajitia kitanzi kujibu
haya wakati yeye ndiye anashikilia makali ya kisu?
Hakuna sababu zaidi ya huruma za kijinga
...ili ndoa zidumu, zinahitajika pia huruma ya "kijinga"
It's all about reasoning power kwa wanandoa.
Ndoa sio mchezo wajameni!
...ili ndoa zidumu, zinahitajika pia huruma ya "kijinga"
It's all about reasoning power kwa wanandoa.
Ndoa sio mchezo wajameni!
...mnh, Lizzy slow down. Ushauri huu unaendana na umri wa watu.
Kuna umri wanaisha bana. Umri ulio "alasiri kuelekea magharibi" inakuwa shughuli kuanza kupenda tena.
Kumbuka, kupenda kunahusisha kujenga msingi, kuta, paa na kwenye; ...urafiki > uaminifu > mazoea >
mapenzi > kushirikiana > kuheshimiana > kufahamiana > nk... na yote haya yanahitaji muda.
..ah haaha!
mara ngapi ushasikia wanandoa wanalalamikiana; "siku hizi simuelewi elewi kabisa mwenzangu, amebadilika!"
mara ngapi ushasikia watu wanasema, "akishaingia kwenye ndoa ndio utaona moto wake!"
Haya ndio yanayotokea ndani ya ndoa. Chaka hilo, huwezi jua miba yake mpaka uupande mchongoma!
BTW, nilimuomba LD atuambie huyo Bi Mkubwa huombaje msamaha.
Kuna wale wanawake wanapoomba msamaha hupiga magoti wakilia mpaka huruma inakujia,
wapo wenye kujiapiza kamwe hawatarudia tena, na huapa bora wajiue kuliko kuishi bila waliyemkosea.
Huruma mama, huruma.
Mbu, wewe kwa mtazamo wako ni hadi ifikie mara ngapi kwa huyo bwana kuchitiwa ndo aamue kutalikiana na mkewe? Au wewe unaona ikija kwenye shauri la ndoa huruma haina kikomo?
Kama mnawatoto wanao hitaji malezi ya baba na mama, dawa kubwa ya kufanya ni kukaa KIMYA baada ya kumuona amerudia kosa kwa mara ya tatu, kukaa kimya sio kumnunia, kukaa kimya unapofanyiwa jambo ambalo sio la kiungwana ni silaha kubwa ya maangamizi maana huenda kupiga ndani ya nafsi ya mtenda kosa. Hivyo kama ana akili timamu atajirudi mwenyewe
Mnataka kwenda wapi aisee!!
Hebu tulieni bwana.
Tunataka njia ya kumwadhibu mwanamke asiye kuwa mtiifu/mwaminifu kwa mume wake,
sio kuwatafutia Desdii na TF BAN bwana wangu!!!
Hicho ndio kiini cha tatizo.Ajisahihishe kama nampenda mdada. Ukute mwanaume mwenyewe anapiga kazi za nje akirudi home kachoka anashindwa kutoa huduma.Iliwahi kumtokea jamaa yangu mmoja.Yeye ana pesa na humpa mkewe kila kitu anachotaka.Lakini jamaa ni mwingi mno wa habari.Hawezi kuridhisha homeground.Matokeo yake mke akachoka akaamua kupata huduma za extension.Sasa jamaa analalamika nini ikiwa anacheza chini ya kiwango?
Via Mobile, nani alikwambia kwamba,
solution ya matatizo ya ndoa ni kuikimbia, au
kuachana?
je,huko utakapopata mwenza mwingine itakuwa ni peponi,
kiasi ambacho hakutakuwa na magomvi tena?
Akuwache uendelee tu, kwani hiyo ina maanisha hakutoshelezi. Kama anakutosheleza huwezi kuwashwashwa.
...ili ndoa zidumu, zinahitajika pia huruma ya "kijinga"
It's all about reasoning power kwa wanandoa.
Ndoa sio mchezo wajameni!
..ah haaha!
mara ngapi ushasikia wanandoa wanalalamikiana; "siku hizi simuelewi elewi kabisa mwenzangu, amebadilika!"
mara ngapi ushasikia watu wanasema, "akishaingia kwenye ndoa ndio utaona moto wake!"
Haya ndio yanayotokea ndani ya ndoa. Chaka hilo, huwezi jua miba yake mpaka uupande mchongoma!
BTW, nilimuomba LD atuambie huyo Bi Mkubwa huombaje msamaha.
Kuna wale wanawake wanapoomba msamaha hupiga magoti wakilia mpaka huruma inakujia,
wapo wenye kujiapiza kamwe hawatarudia tena, na huapa bora wajiue kuliko kuishi bila waliyemkosea.
Huruma mama, huruma.
Ndugu yangu Mbu,
Una maana ukianzisha biashara (na hiyo ndo kazi yako unayoijua) ikafilisika unajiua? Why not start again?