Kuna muda ubahili una gharama kubwa sana, ni kitu gani umewahi kujibana kikakugharimu zaidi ?

Kuna muda ubahili una gharama kubwa sana, ni kitu gani umewahi kujibana kikakugharimu zaidi ?

Mwaka2021 nilkuwa na tupesa twachuoni nikiwa naplan ya kuanzisha biashara.nilijibana sana ila kwabaadae nikiwa nataka kufungua biashara akafa babu na om hawakuwa na hela. Ikabidi mama aniombe hizo pesa kwa kigezo tutarudisha ili zifanye mazishi. Hadi leo sijalipwa na nlipopata kazi ndo nikasamehe lkn nilipitia ugumu mwingi sana kiasi chakusema si bora ningekula bata humo chuo
 
Hizi simu za shortcut zimetupeleka ling cut sana kuanzia kununua,matengenezo n.k
Kwa sasa sinunui simu mkononi/used au kupeleka kwa fundi.
Nina masimu kibao yameharibika hapa na naona tatzo dogo ila sipeleki.Ni either nitumie hvyo hvyo au ninunue mpya.
 
Kuna muda huwa tunabana pesa aidha kwa kununua bidhaa zilizotumika, bidhaa zenye ubora mdogo, kununua kitu cha dili, kujaribu kutumia bidhaa mbadala, n.k.lakini consequences zinatugharimu sana.

Nilikuwa na laptop yangu, upande wa hard disk umelegea, matengenezo ni elf 15, nikajifanya mjuaji nikaweka ufuto uibane hard disk, siku moja nimepeleka laptop kwa fundi, vile ameifungua tu hard disk ikadondoka na ikafa papo hapo, kumbukumbu zooooote za picha, videos, nyaraka, n.k. vilikwenda moja kwa moja, hata niwe na milioni siwezi kuvipata tena

Nilipoweza kumiliki gari niliwahi kujifanya mjuaji nikaweka mafuta ya breki kwenye sehemu ya kuweka mafuta ya usukani, sikuona haja ya kuleta fundi ili ni save pesa, kilichotokea niligharamika 150,000 kutengeneza usukani, wakati ningeenda kwa fundi ushauri na maelekezo visingezidi elf 5.
Kuna mambo mengine sio ubakhili ni ujinga, binafsi napenda mambo yalio nyooka sio kuunga unga kama nahitaji kitu basi ntanunua kihalili kabisa

Kuhepusha usumbufu baadae
 
Mwaka2021 nilkuwa na tupesa twachuoni nikiwa naplan ya kuanzisha biashara.nilijibana sana ila kwabaadae nikiwa nataka kufungua biashara akafa babu na om hawakuwa na hela. Ikabidi mama aniombe hizo pesa kwa kigezo tutarudisha ili zifanye mazishi. Hadi leo sijalipwa na nlipopata kazi ndo nikasamehe lkn nilipitia ugumu mwingi sana kiasi chakusema si bora ningekula bata humo chuo
[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Mwaka2021 nilkuwa na tupesa twachuoni nikiwa naplan ya kuanzisha biashara.nilijibana sana ila kwabaadae nikiwa nataka kufungua biashara akafa babu na om hawakuwa na hela. Ikabidi mama aniombe hizo pesa kwa kigezo tutarudisha ili zifanye mazishi. Hadi leo sijalipwa na nlipopata kazi ndo nikasamehe lkn nilipitia ugumu mwingi sana kiasi chakusema si bora ningekula bata humo chuo
Hakua baba yako mzazi?!
 
Nilikua natoka harusini mbezi Magufuli mida kama saa nane usiku.

Nikaangalia geji naona imeshuka kichizi, mfukoni nina cash 15k pekee, nilipofika goba, petrol station ⛽naiona ileee akili ikaniambia hayo mafuta unafika nayo home acha ufala usiende kujaza mengine, hiyo 15000 itakusaidia mishe nyingine kesho.

Kweli bhana nikaghairi, nikaona hapa napita njia shotikati ya goba ndani ndani kisha natokea home salasala.

Kuna kinjia kimoja unavuka mto, halafu unapandisha kilima kireeeefu, ukimaliza tu unaibukia kinzudi.

Nikavuka mto, ile naanza kupanda kilima nafika nusu chombo ikazima mafuta yamerudi nyuma kutokana na ule mwinuko, nikaishusha chombo mdogo mdogo coz imezima, nilipofika chini kabisa kule mtoni nikaiwasha ikawaka.

Kutia gia naanza kupanda chombo ikazima tena na haikukubali kuwaka teeena, hapo ni saa nane usiku na madakika yake, chombo iko mtoni katikati, simu imezima chaji(matokeo ya kurekodi video harusini).

Nikaona ni bora nitembee kupandisha juu upande wa pili labda naeza kukutana na boda holaaaa, nikatembea mpaka sehemu inaitwa usukumani, nikamkuta mmoja alitea abiria ndio anageuza

Nikamstopisha nikamuelekeza nataka kwenda kununua mafuta, akataka buku nne kwenda na kurudi safari ikawa ni Africana, nikawaza niende nae niiache gari mtoni, hapana

Nikamwambia aende akanunue kwa hela yake akija nampa akasema hana hela zaidi ya buku 2, Nikawaza nikimpa ten langu akaenda mazima asirudi itakuaje?

Nikawaaaza nikaona poa tu, ngoja niende nae, kwanza saiv usiku wa manane nani atakua na uthubutu kwenda kufungua kitu kwenye gari iliyopaki mtoni tena panatisha *******.

Nikapanda boda sie haooooo, ama kweli siku ya kufa nyani miti yoote huteleza, yaani kabla hata ya kufika sheli, booooooonge la mvua likaanza kunyesha, boda akapaki pembeni kujikinga na mvua.

Hapo tayari mie nikaanza kupaniki maana najua gari iko katikati ya mto na kuna boonge la mvua, nikaanza kukimbia na ile mvua naenda sheli sasa, kufika jamaa akaniwekea mafuta ya 10k kwenye kidumu.

Kila boda ninaemgusa anipeleke ananiuliza kwani wewe huoni hii mvua??

Nikaona huu upuuzi nikaanza jogging kupandisha kuiwahi gari isije kubebwa na maji, mvua ilipopungua kuna boda mmoja ndio akaja kwa huruma tu akanikuta njiani nakimbia akanipakia haooo mpaka eneo la tukio.

Nafika kwenye gari nikakuta maji kama yoote, gari imepigwa mtama kitoogo kwa nyuma, ndio ilikua inasogezwa kidogo kidogo na maji, imeanza kugeuka kabisaa upande wa nyuma unaelekea uelekeo wa maji yanapoenda, nikakuta majani, mamiti na matakataka mingine yaliyobebwa na maji kutoka huko yamejaa ubavuni mwa gari.

Bila kusita nikajitosa kwenye maji nikazama ndani ya gari, nikachukua kamba, nikafunga ile sehemu ya kuvutia gari kisha nikaenda kuifunga kamba kwenye mti, ili hata kama gari itazidiwa na maji kuanza kuondoka basi ile kamba inaweza hata kunisaidia kuichelewesha gari isiondoke mapema.

Baada ya hapo nikajaza mafuta, washa washa na wewe, aaaaah wapi, washa mpaka bettri inanyonya chuma haipokei inazidi kusogezwa na maji mdogo mdogo mpaka ile kamba ikakaza nikajua hapa kamba ikikatika tu, gari imeenda na maji.


Asubuhi saa 12 ndio gari za mchanga zikaja kunisopoa, kuivuta gari stendi ya kwanza gereji, pesa iliyonitoka ni siri yangu aiseeee lakini nilijilaumu sanq kwa uzembe
😂😂😂nimechek balaaa nikiwa huku kijijini
 
Niliacha kupanda shuttle shilingi 400 toka mabibo hostel hadi UDSM siku ya paper, wakati wa ukaguzi kuingia kwenye mtihani nikajikuta nilichukua ID ya mpiga kura badala ya ile ya chuo.

Ilibidi nilipe boda 8000 kuifuata ili aokoe muda
 
Nilikuwa na laptop yangu, upande wa hard disk umelegea, matengenezo ni elf 15, nikajifanya mjuaji nikaweka ufuto uibane hard disk, siku moja nimepeleka laptop kwa fundi, vile ameifungua tu hard disk ikadondoka na ikafa papo hapo, kumbukumbu zooooote za picha, videos, nyaraka, n.k. vilikwenda moja kwa moja, hata niwe na milioni siwezi kuvipata tena

Nilipoweza kumiliki gari niliwahi kujifanya mjuaji nikaweka mafuta ya breki kwenye sehemu ya kuweka mafuta ya usukani, sikuona haja ya kuleta fundi ili ni save pesa, kilichotokea niligharamika 150,000 kutengeneza usukani, wakati ningeenda kwa fundi ushauri na maelekezo visingezidi elf 5.
Laptop hii kitu imepita na wengi Aisee .mpaka Kesho nikiitaji la laptop naenda kununua mpya .


Kupiga window na maintenance nyingine naenda Kwa fundi mbobezi tena nakaa naye kabisa .
 
Ugwadu ulinikaba, kichwani pombe, nikataka chochote cha kufanya nipizi. Kwa ubahili, nikajishawishi nipate walau bj kwa madada poa wa buku kumi badala ya wale wa 15k - 20k.
Bwana weeh! Niliishia kuibiwa pesa taslimu na simu.
Nikaachana na mambo ya madada poa tokea hapo.

PS: Bao nilipiga 😄
 
Laptop hii kitu imepita na wengi Aisee .mpaka Kesho nikiitaji la laptop naenda kununua mpya .


Kupiga window na maintenance nyingine naenda Kwa fundi mbobezi tena nakaa naye kabisa .
Hapa nifanye ku copy documents zoote za kwenye SIMU. Maana na simu mbili pia email yangu imejaa Sanaa

Nizihamishie kwenye sehemu salama yasije Nikuta maana hii simu moja imeanza kuchoka na ndio ofisi yenyewe..

Isije ikafa nikakosa back up
 
Back
Top Bottom