Kuna nafasi hazijawahi kutwaliwa na wanawake, Makamu mwenyekiti CCM na Katibu mkuu CCM, kwanini?

Nanye Go

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
10,856
Reaction score
14,607
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, sijawahi kusikia makamu mwenyekiti ccm mwanamke, pia Katibu mkuu ccm mwananmke.

Tumeona makamu wa rais mwanamke na akawa rais ki bahati bahati tu. Hizo nafasi haziwezi kutwaliwa na mwanamke huko ccm? vipi katibu mkuu ccm haiwezekani akapewa mwanamke pia?

Haya sasa Chongolo alijiuzulu mwenyewe, kwanini wanaosemwa kuirithi nafasi yake ni wanaume watupu?
CCM waachieni mama zetu labda tutabahatisha anayeweza.
 
Naunga mkono hoja
P
 
Tega sikio kwa makini!
 
Kwani huko chadema hali ikoje? Lini wanawake walishika hizo nafasi? Acha kujitoa ufahamu.,
 
Baada ya kupata Katibu Mwenezi mwanamke sasa tungepata mwanamke kama Katibu Mkuu.Wapo kinamama wanatosha.
Nilishapendekeza mwanamke anayefaa ila nikaambiwa the odds against a woman kuwa katibu mkuu,mara mzee,mara akabond na mumewe,mwishowe ni jinsia tu.
 
Wajitokeze,wakikidhi vigezo,watapewa au wanasubiri mbeleko?
Akina Sophia Mjema walipewa nafasi,lakini walilegalega,sijajua wakipewa huo u-KM itakuaje.

 
Hii dunia imeumbwa kwa ajili ya mfumo dume. Na ni ukweli kwamba wanaume pekee wanapaswa kuwa ndiyo watawala.

Fanya utafiti katika jamii zote za wanyama, kwa kuwa binadsmu yupo katika kundi hili la kibaolojia. Huwezi kukuta mahali popote pale kiongozi wa kundi ama familia ni mwanamke.

Ni makosa makubwa sana kumuweka mwanamke awe juu kiutawala katika majukumu nyeti ya utawala, labda iwe kwa ajili ya kuwa "figurehead" tu. Kufanya mwanamke kuwa mtawala ili upate matokeo chanya, hakuna tofauti yoyote ile na kucheza kamari.
 
Mna mwenyekiti, mnataka na makamu na katibu mkuu? Mlijaribishwa mwenezi mkafeli
 
CCM ni Chanzo Cha Matatizo
 
Nafasi za wala nchi
 
Hata kwenye taasisi za umma nafasi za CEOs na HOD zitangazwe ndani ya taasisi husika watu waombe wapite kwenye ushindani huru .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…