kuna ujumbe unasambazwa kwenye makundi ya whatsapp ukidai kuwa kuna namba ikikupigia ama kutuma ujumbe na ukijibu unapoteza maisha kwani mtumiji wa namba hiyo anatafuta damu za watu ni kweli?
- Tunachokijua
- Kumekuwepo na ujumbe mfupi wa maandishi unaosambazwa kwenye makundi ya Whatsapp ukiwatahadharisha watu kuhushu uwepo wa namba ya simu inayotuma ujumbe ama kupigia simu watu, na wale watakaoujibu ujumbe huo ama kupokea simu kutoka kwenye namba hiyo wanapoteza maisha, na watu 12 wameshapoteza maisha kutokana na kujibu ama kupokea simu kutoka kwenye namba hiyo.
Ujumbe huo pia unaeleza kuwa anayetumia namba hiyo ni mwanamke ambaye lengo lake ni kuwanyonya watu damu.
Ukweli upoje?
JamiiCheck imeuchunguza ujumbe huo na kubaini si wa kweli kwani taarifa hiyo imeeleza kuwa vifo 12 vilivyotokana na suala hilo imetangazwa “Leo saa mbili” kwenye shirika la habari TBC, ujumbe unasema kuwa taarifa imetangazwa “Leo’’ lakini haujaweka tarehe husika ya suala hilo lilipotangazwa hivyo kuleta changamoto ya kubaini “Leo” inayozungumziwa ni ipi? Lakini pia ujumbe haujaeleza hivyo vifo vimetokea wapi na lini, na waliofariki ni akina nani.
Ujumbe huo umeweka namba ya simu inayotumika na anayedaiwa kuwa mnyonya damu lakini namba hiyo ni pungufu kwa ina namba tisa badala ya kumi kama ilivyo kwa namba nyingine.
JamiiCheck imeipigia namba hiyo na majibu yalikuwa kwamba "Namba hiyo haipo tafadhali hakikisha namba na ujaribu tena."
JamiiCheck imewasiliana pia na Shirika la utangazaji Tanzania (TBC) kupitia kwa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano cha shirika hilo Catherine Nchimbi kupata uhalisia kama wameshawahi kutoa taarifa hiyo ambapo amesema kuwa tarrifa hiyo uzushi na imekuwepo kwa muda mrefu.