Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Wakuu nahisi huyu ndugu babu talent kuna nguvu ya ziada anaitumia si bure.
Nimejaribu kufatilia kwa karibu kabisa wasanii waliokuwepo chini yake na baadaye kwa namna moja au nyingine wakaachana naye hasa kuachana naye katika mazingira ambayo sio mazuri ,wengi wao kama sio wote wanapotea kabisa kwenye ramani ya mziki na hawasikiki tena ,ngoja nikutolee mfano wa wanamuziki waliokuwepo chini yake na baadaye wakaachana naye na kupotea mazima ;
1)MB Doggy
huyu jamaa alikuwa na ngoma kali sana kama vile Latifa ,Si uliniambia ,Sagablasha nk lakini baada ya kuachana na mzee talent tu basi akapotea mazima kwenye mziki .
2)Z _Anto
huyu jamaa alitamba sana na ngoma kali kama vile binti kiziwi ,Jini jini,nk lakini baada ya kukorofishana na tale basi huo ndio ukawa mwisho wake wa muziki ,alipoachana na tale Z _ANTO alihamia kwenye kuimba taarabu ambako alizidi kujichimbia kaburi lake kwenye ramani ya mziki na mwisho wa siku hata aliporudi kwenye kuimba bongo fleva bado hakufanikiwa kufanya lolote lile .
Mbali na Z anto wengine waliopotea kwenye mziki ni kama vile
3)Pingu na mwenzake Deso
4)Spark
5)PNC ingawaje mwanzoni alijitahidi lakini baada ya muda akapotea mazima.
Hivyo basi napenda kutoa angalizo kwa bwana mdogo Diamond Platinumz awe makini sana na huyu jamaa kwani wakiachana tu jamaa hatotaka faida alizokuwa anapata kipindi yupo na mondi mwengine azipate hivyo basi atafanya juu chini kumpoteza mondi
Huu ni mtazamo tu naweza kuwa nipo sahihi au lah
Hivyo kwa namna moja au nyingine ningependa nisikie/kuona mawazo kutoka kwenu wanajamvi wenzangu.