Kuna nini Azam na mwendo huu wa kuchechemea

Kuna nini Azam na mwendo huu wa kuchechemea

Sodoku

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2016
Posts
1,271
Reaction score
2,903
Hii ndiyo Club tajiri kwa hapa Tanzania. Najiuliza wamepatwa na nini? Uwanja wanao mzuri tu.

Pesa na matunzo mazuri wanayo. Tatizo ni nini?
 
Pengo la Kipe tcheche linaonekana dhahiri,hawakutafuta mbadala,Wawa hana mbadala pia na Kapombe ni majeruhi,ndio madhara ya kuwa na kikosi ambacho baadhi ya watu wasipokuwepo basi timu haipati matokeo
 
Mi naona kubadili Kocha ndiko kunakowasumbua Azam,na waangalie wanaweza kushuka daraja kama wakichukulia poa mwenendo wao.
 
Hii ndiyo Club tajiri kwa hapa Tanzania. Najiuliza wamepatwa na nini? Uwanja wanao mzuri tu.

Pesa na matunzo mazuri wanayo. Tatizo ni nini?

Pale AZAM ilipochukua kombe la klabu bingwa Afrika mashariki nilimsikia dogo yule ambaye ni mtendaji mkuu wa AZAM akitamba kuwa sasa wale (klabu) ambao walidhani soka ya Tanzania ni miliki yao watambue kuwa AZAM imefika wapende au wasipende...yalikuwa ni maneno ya majigambo na ambayo kwa maoni yangu yalikuwa premature, baadhi yetu tulinyamaza kimya....AZAM sasa ameanza kuisoma namba na Jumapili ataendelea kuisoma namba ....
 
Azam pale kuna figisu tena sana tu nani wa kuamin HALL aliondolewa pale kwasababu ana uwezo mdogo?
 
Soka la spain na Africa wapi na wapi?Hapo ndipo azam waliingia choo cha kike.Walau wangeenda serbia hao tunafanana nao philosofia za mpira.
 
Ila hawajachelewa.piga chini kocha then nenda serbia hapo vuta kifaa na mwisho watafute straika mmoja wa ukweli.wakifanya hivyo raundi ya pili ni kuteleza tu.
 
Kosa wanalofanya Azam ni kununua wachezaji toka Simba na Yanga, siku zote wachezaji wa Sunche na Kapeto wanaangalia maslahi zaidi kuliko mapenzi na timu, Azam wana academic nzuri waanayoweza kuitumia kuunda timu ya wakubwa na ikawa tishio Africa.
 
Hii ndiyo Club tajiri kwa hapa Tanzania. Najiuliza wamepatwa na nini? Uwanja wanao mzuri tu.

Pesa na matunzo mazuri wanayo. Tatizo ni nini?
Kesho watamuoshea nyota Yeboyebo 3 - 1
 
Hii timu wafukuze benchi la ufundi wote wanatafuna hela tu hawatupi raha mashabiki zao,mana kikosi bado ni kizuri...na uongozi wa Azam FC bado wananishangaza inamaana mpaka leo hawajui jinsi ya kuchagua makocha wanaofaa..
 
Back
Top Bottom