kisale
Senior Member
- Mar 3, 2009
- 111
- 1
Baraza la Mitihania ni Taasisi iliyo chini ya wizara ya Elimu na Mafunzo,kwa namna moja au nyingine ni moja ya wizara nyeti sana nchini kwetu Tanzania.Kuna kitu kimoja kati ya vingi kinachokera sana katika utendaji wa taasisi hii ya serikali,ni miaka ya karibuni tu baraza limebadilisha utaratibu kwa watahiniwa kuchukua Result slip zao kutoka baraza la mitihani na kuwapa jukumu hilo taasisi nyingine ya serikali ambayo ni Posta Tanzania.kipindi cha nyumba ilikuwa ukienda baraza na ukafanikiwa kujaza form kuomba result slip kabla ya saa 4 asubuhi utaambiwa muda wowote baada ya saa7 mchana ukachukue,na ukijaza baada ya saa 4 asubuhi itatakiwa uende kuchukua siku inayofuata.Kwa kile wao walichokiita kuboresha huduma kwa watahiniwa,kwa sasa ukitaka result slip utatakiwa uende Posta ujaze form na kulipia,na badala ya kulipia 5000 kama ilivyoidhinishwa na baraza utatakiwa kulipa 8000 ambayo inajumuisha na gharama za posta.kinachokera zaidi utaambiwa ukafuate slip yako baada ya siku 14,na wakati mwingine ukienda utaambiwa baraza bado hawajatuma hizo slip njoo siku nyingine ukiwauliza kwanini zimecheweshwa utaambiwa wao sio baraza la mtihani.Sasa tujiulize nini hasa nia ya baraza la mitihani kuhamishia hiyo huduma posta?ni ili kuzidi kuwaibia walala hoi visenti vyao vichache kwa kuwaongezea gharama,au ni furaha yao kuona Mtanzania unahangaika kwa mwezi mzima kwa huduma ambayo kiukweli haiwezi kuzidi dk 5 kama Baraza wataamua, kwa sababu ni kiasi cha mtu kujaza form wao kazi kuprint na kusaini mhusika tu.Nini kifanyike kuondoa uozo huu baraza la mitihani?