Kuna nini Baraza la Mitihani Tanzania?

Kuna nini Baraza la Mitihani Tanzania?

kisale

Senior Member
Joined
Mar 3, 2009
Posts
111
Reaction score
1
Baraza la Mitihania ni Taasisi iliyo chini ya wizara ya Elimu na Mafunzo,kwa namna moja au nyingine ni moja ya wizara nyeti sana nchini kwetu Tanzania.Kuna kitu kimoja kati ya vingi kinachokera sana katika utendaji wa taasisi hii ya serikali,ni miaka ya karibuni tu baraza limebadilisha utaratibu kwa watahiniwa kuchukua Result slip zao kutoka baraza la mitihani na kuwapa jukumu hilo taasisi nyingine ya serikali ambayo ni Posta Tanzania.kipindi cha nyumba ilikuwa ukienda baraza na ukafanikiwa kujaza form kuomba result slip kabla ya saa 4 asubuhi utaambiwa muda wowote baada ya saa7 mchana ukachukue,na ukijaza baada ya saa 4 asubuhi itatakiwa uende kuchukua siku inayofuata.Kwa kile wao walichokiita kuboresha huduma kwa watahiniwa,kwa sasa ukitaka result slip utatakiwa uende Posta ujaze form na kulipia,na badala ya kulipia 5000 kama ilivyoidhinishwa na baraza utatakiwa kulipa 8000 ambayo inajumuisha na gharama za posta.kinachokera zaidi utaambiwa ukafuate slip yako baada ya siku 14,na wakati mwingine ukienda utaambiwa baraza bado hawajatuma hizo slip njoo siku nyingine ukiwauliza kwanini zimecheweshwa utaambiwa wao sio baraza la mtihani.Sasa tujiulize nini hasa nia ya baraza la mitihani kuhamishia hiyo huduma posta?ni ili kuzidi kuwaibia walala hoi visenti vyao vichache kwa kuwaongezea gharama,au ni furaha yao kuona Mtanzania unahangaika kwa mwezi mzima kwa huduma ambayo kiukweli haiwezi kuzidi dk 5 kama Baraza wataamua, kwa sababu ni kiasi cha mtu kujaza form wao kazi kuprint na kusaini mhusika tu.Nini kifanyike kuondoa uozo huu baraza la mitihani?
 
Mkuu Kisale, heshima mbele

Ninavyofikiria mimi moja ya kufanya hudumu kuwa za wepesi kwa wenye kuamini utawala bora na kupunguza urasimu ndio maana imefanyika hiyo Decentralization kwahiyo nafikiri ile biashara na mazoea ya kwenda pale na kusongamana labda wameona mnapata tabu ndio maana wameona kufanya hivyo. Mawazo tuu
 
kwa kifupi Dr NDALICHAKO kazi imemshinda anendesha ofisi kama Grocery, ameajiri watu wasio makini kiutendaji e.g Daniel Mafie Director of Administration pamoja na Kihanga Human resouce office, waha ndio wanoliangusha baraza la mitihani kazi yao kufukuza watu kazi bila sababu za msingi,na kabda ya kuajiriwa hapo wote wawili walikuwa wafanyakazi wa National Institute for Medical Reserch huko nako walifanya madudu wakakimbilia baraza la mitihani sehemu nyeti kupavuruga
 
Tatizo serikali imelala usinzingi mzito,...........hata syetem nayo hakuna kitu
 
Tatizo serikali imelala usinzingi mzito,...........hata syetem nayo hakuna kitu

hehehe
kama system nao waingilie suala la elimu basi ngoma nzito.
hapa ni kwamba wasomi wangi wa kitanzania si halisi ndo maana wakipewa nafasi wanaharibu hata msingi wenyewe. Nina doubt hata wale wasomi ambao wamepitia vyuo vinavyotambulika na serikali wengi bado ni vilaza.
Nyerere alisema kwamba kadiri mtu anavyozidi kuelimika, asipokuwa mwangalifu ndivyo anavyozidi kuwa mjinga...
 
mmasaihalisi nakuunga mkono 100%hao jamaa wawili kazi yao kufukuza watu kazi nakuwazibia wasiende shule kusoma ukiomba kwenda shule hata kama unajilipia mwenyewe kosa,huyo Kihanga kwa uchunguzi niliofanya nasikia ni MTUSI,sijui kapata lini urai wa Tanzania
 
kwa kifupi Dr NDALICHAKO kazi imemshinda anendesha ofisi kama Grocery, ameajiri watu wasio makini kiutendaji e.g Daniel Mafie Director of Administration pamoja na Kihanga Human resouce office, waha ndio wanoliangusha baraza la mitihani kazi yao kufukuza watu kazi bila sababu za msingi,na kabda ya kuajiriwa hapo wote wawili walikuwa wafanyakazi wa National Institute for Medical Reserch huko nako walifanya madudu wakakimbilia baraza la mitihani sehemu nyeti kupavuruga

Nadhani NECTA ina directorates na departments, Swali langu ni kwamba uandaaji na utumaji wa hizo slips upo chini ya Directorate ya bwana Mafie? Je ni KWELI PIA INAANGUKIA KATIKA DEPARTMENT YA HR?

Binafsi sina hapa organizationa structure ya NECTA na sijajua majukumu ya kila directorate kama yupo anyefahamu vema ATUBANDIKIE HAPA ili tumlenge muhusika halisi.

Lakini kwa jinsi na namna yoyote ile huyo CEO anatakiwa awe responsible
Hii inakera sana sana.
 
Back
Top Bottom