The last don
JF-Expert Member
- Aug 3, 2011
- 1,053
- 1,232
Nakumbuka Zola alikuwepo kwenye kikosi cha Azzuri World cup 94,akapigwa red card katika mechi yao na Nigeria,nadhani kuanzia hapo hakuweza tena kupata nafasi katika National team.Sio jambo geni katika soka.
Dunia ya soka iliwahi kumshuhudia Eric Cantona akiwa wa moto kabisa pale Man Utd lakini timu ya taifa ya Ufaransa alikuwa haitwi.
Gianfranco Zola akiwa mungu mtu pale Chelsea kiasi cha kwamba jezi yake namba 25 kustaafishwa isitumike tena Chelsea, timu ya taifa ya Italy (Azzuri) alikuwa anaisikia kwenye bomba.