Tetesi: Kuna nini kati Ya Maalim Self na Utawala wa Sultan uliopinduliwa Zamani Zanzibar!!

Tetesi: Kuna nini kati Ya Maalim Self na Utawala wa Sultan uliopinduliwa Zamani Zanzibar!!

Wadau ni mda mrefu sasa kumekua na habari mtaani.Kwamba Cuf au Maalim Self wakipewa Nchi ya Zanzibar .Wale waarabu na Ukoo wa Sultan watarudi kuitawala tena Zanzibar.Na hii ndio sababu CCM hawako tayari kuwapa nchi hata kama wanashinda uchaguzi.Na kwa nini Maalim Self hataki kutoka hadharani kufafanua juu ya hii ishu kwani ipo na ina semwa sana toka kitambo.CCM Zanzibar wamesha sema kua nchi iliyo patikana kwa mapinduzi hawawezi kuikabidhi kwa Makaratasi.Viongozi wa Cuf Zanzibar pamoja Na Maalim Self tunaomba ufafanuzi juu ya hili..
Mkuu Reformer, karibu tembelea nyuzi hizi ili ujielimishe mambo ya Zanzibar!.
Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano
Ni nini kinachosumbua Maalim Seif?
Imethibitishwa pasi na shaka Maalim Seif Alishinda Zanzibar
Jee Kuna Uwezekano Siku Zote Huwa Hazitoshi, Bali Zinatosheshwa

Pasco
 
Kiukwli siasa ya Zanzibar ni zaidi ya u cuf na u ccm tunahaja ya kuendelea kuiamini ccm zaid kuliko kutafta uchchezi
 
Ukweli ndio utakao tuweka huru.Ni vzur Maalim self mwenyewe..Akalitolea jambo hili ufafanuz kuliko kuwa kimya.Wazanzibar wanahitaji permanent solution sio kufunika kombe
Maalim seif ameshawahi kusema kuhusu hilo.
Amesema" Salmini ndiye aliye mkaribisha Jamshid Zanzibar na Kampa kibali cha kuja kuishi au kutembea "
Salmini aliyasema haya wakati alikua na njama kutaka kutawala vipindi zaidi ya viwili.

Ufalme ulotawala Zanzibar na ule ulokuwepo Oman ni vitu viwili tafauti. Mfalme wa Zanzibar alipo hama hakuweza kwenda Oman lakini alikwenda UK.

Sasa huyo anayetaka kurejeshwa yukowapi?
 
NISAHIHISHE MKUU JE CUF WANAMTAZAMO GANI KUHUSU MAPINDUZI YA JANAURI 12, WANAMTIZAMO GANI KUHUSU SULTAN SEYYID JAMSHID BIN SAID AL BUSAID.
Hizo ni propaganda za kitoto kabisa zinazoendeshwa na wanaccm.

Mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika zaidi ya miaka 50 iliyopita, leo hii baada ya kipindi kirefu chote hicho wanaccm wanaendelea kupandikiza mbegu za chuki ndani ya wazanzibari kwa kupitisha mabango yao ya kichochezi mbele ya Shein na huyo mama Samia, kwenye sherehe za mapinduzi za mwaka huu yanayosomeka CHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI YA WAAFRIKA PEKEE.

Cha kushangaza kupita kiasi wakati vijana wale wa UVCCM wakipita kwenye jukwaa kuu kwenye sherehe hizo, viongozi wote wa ngazi za juu wa chama hicho waliokuwa kwenye jukwaa kuu walikuwa wakishangilia kwa kupiga makofi huku wakikenua meno!

Niwakumbushe kidogo tu historia hao viongozi wahafidhina wa CCM wa huko Zenji kuwa hata yale mauaji ya kimbari yaliyotokea kule Rwanda mwaka 1994 yalisababishwa na 'cheche' za dizaini hii hii inayopandikizwa na wahafidhina wa CCM wa nchi hii.

Tunapaswa watanzania wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa kukemea kwa nguvu zetu zote mchezo huu hatari sana wa kibaguzi unaochezwa na wanaccm kwa lengo moja tu la kujihakikishia kuwa wanaendelea kuitawala nchi hii hadi mwisho wa dunia.

Iwapo watanzania tutafumbia macho vitendo hivyo vya kipuuzi vinavyofanywa na wanaccm, pale nchi yetu itakakuja kuangamia haitabagua na kuwaacha wanaccm na kuwaangamiza wapinzani pekee, kiuhalisia wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, SOTE KABISA TUTAANGAMIA.
 
Wadau ni mda mrefu sasa kumekua na habari mtaani.Kwamba Cuf au Maalim Self wakipewa Nchi ya Zanzibar .Wale waarabu na Ukoo wa Sultan watarudi kuitawala tena Zanzibar.Na hii ndio sababu CCM hawako tayari kuwapa nchi hata kama wanashinda uchaguzi.Na kwa nini Maalim Self hataki kutoka hadharani kufafanua juu ya hii ishu kwani ipo na ina semwa sana toka kitambo.CCM Zanzibar wamesha sema kua nchi iliyo patikana kwa mapinduzi hawawezi kuikabidhi kwa Makaratasi.Viongozi wa Cuf Zanzibar pamoja Na Maalim Self tunaomba ufafanuzi juu ya hili..
Link Mapinduzi ya Pili Zanzibar
 
Walikua wana muonea Bure Maalim wakati wenye wajomba zao arabuni ni wengi na likizo wanaenda huko o
 
Back
Top Bottom