Hizo gari chakavu mnazonunua ambazo zina pollute mazingira huwa mnazifikiria?Naomba nipinge kwa nguvu hoja yako hapa
Kwani shida kubwa ya Afrika ni umeme pekee??
Kwani chanzo Cha nishati kwa Afrika nzima ni HEP pekee??
Hiyo hadithi ya River congo Hydroelectricity power kuwa ingekuja kusapply umeme umeiitoa wapii??
Stiglarz hainuki uharibifu wa mazingira hadi mvua za vuli kukosekana ukanda huo wa Morogoro????
Tusijaribu kuwapa majina mabaya wanaotushauri
Je, ukweli ndio huu?
Vita ya mradi wa Rufiji sio ya kwanza Afrika (Dr Yahya Msangi (Phd), Togo West Afrika)
"HUENDA wengi hawajui visa vya mabwawa ya kufua umeme na historia ya Afrika. Nimeona bora niwaelimishe. Mabwawa haya yana kitu kinaitwa 'geo-politics' toka zamani na yapo mabwawa ambayo yamewahi kuhujumiwa ili yasijengwe
http://www.ituc-africa.orgYahya Msangi. Regional coordinator of Occupational Safety, Health and Environment (OSHE) at ITUC Africa in Lome, Togo
Zinazopingwa ni facts katika maelezo hayo. Mfano: hivi huyo Lumumba aliyetawala kwa muda wa miezi mitatu tu tena katika vita vya kugombea utawala, alipata muda gani kushughulikia hatua za ujenzi wa hilo bwawa la mto congo?Hii mada japo umeeleza ukwel lkn kuna machawa na mabwege yatakuja kupinga as if yanaundugu na hao watu weupe..wanaharakati ni watu wa hovyo sana
Zinazopingwa ni facts katika maelezo hayo. Mfano: hivi huyo Lumumba aliyetawala kwa muda wa miezi mitatu tu tena katika vita vya kugombea utawala, alipata muda gani kushughulikia hatua za ujenzi wa hilo bwawa la mto congo?
Na haya mabwawa mengine yalijengwa kabla au baada ya ukoloni?
CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM | Facebook
Na Dr Yahya Msangi (Phd) Togo West Afrika ... Mto Congo (DRC), Jinja (Uganda) na Stiegler's Gorge (Tanzania). ... Bwawa la mto Kongo na Stiegler's
Asante Mwengeso kwa mada hii.Kwa uongozi tulio-nao sasa na background yake(from NGOs) na main backer wao(Kikwete),sina shaka yeyote kwamba hii ni kweli.Time will tell,ilà mficha maradhi kifo humuumbua.Wataumbuka tu.Mengi yamezungumzwa kuhusu ujenzi wa hilo Bwawa. La hivi karibuni ni pale Waziri husika alipodai mkondrasi wa ujenzi, ambaye ana utaalamu, ujuzi, uzoefu na uwezo mkubwa, ati hana mtambo wa kubeba (winch) wenye uwezo wa kusimika milango ya kuzuia maji yenye uzito wa tani 26. Au ni hadithi ile ile ya wasiotaka bwawa hilo lijengwe.
Je, ukweli ndio huu?
Vita ya mradi wa Rufiji sio ya kwanza Afrika (Dr Yahya Msangi (Phd), Togo West Afrika)
"HUENDA wengi hawajui visa vya mabwawa ya kufua umeme na historia ya Afrika. Nimeona bora niwaelimishe. Mabwawa haya yana kitu kinaitwa 'geo-politics' toka zamani na yapo mabwawa ambayo yamewahi kuhujumiwa ili yasijengwe. Miongoni mwa mabwawa hayo ni Cahora Bassa (Msumbiji/Afrika Kusini) Aswan (Misri) Akosombo (Ghana), Blue Nile (Ethiopia), Mto Congo (DRC), Jinja (Uganda) na Stiegler’s Gorge (Tanzania).
Kati ya haya mabwawa saba, mawili yalishindikana kujengwa kutokana na ‘geopolitics.’ Bwawa la mto Kongo na Stiegler’s. Nchini Kongo Patrice Lumumba ambaye alitoa kipaumbele kikubwa na kuonyesha nia thabiti ya kujenga bwawa kubwa kabisa (urefu maili mbili) kukinga maji ya Mto Kongo, aliuawa kikatili na mradi husika ulikwama.
Bwawa lile kama lingefanikiwa kujengwa, lingekidhi mahitaji yote ya umeme Afrika na Ulaya na bado kungekuwa na ziada. Sehemu ambapo bwawa hili lingejengwa, ndio yenye maji mengi na yaendayo kwa kasi zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote duniani. Lumumba angefanikiwa, kusingekuwa na haja ya nchi nyingine yoyote Afrika kujenga bwawa au kununua mitambo ya kufua umeme.
Kwa kuzuia ujenzi wa bwawa lile, mabeberu walifanikiwa kuzuia maendeleo ya bara zima la Afrika, kwani kusingekuwa na kijiji au nyumba Afrika ingekosa umeme. Viwanda vingechomoza mpaka vijijini.
Afrika ilizuiwa wakati Ulaya iliyotoka kwenye vita ikiruhusiwa kujenga mabwawa tena ya kuchangia! Sababu kubwa ikipigiwa chapuo ni kuwa, mradi utakuwa na hasara na kwamba Kongo haikuwa na uwezo kutekeleza mradi ule!
Ilipofika zamu ya Stiegler’s hadithi ikabadilishwa. Si tu kwamba uchumi wa Tanzania haumudu mradi huo (japo Cuba na China walijitolea) ikaingizwa hadithi ya uhifadhi vyura na vipepeo! Eti, itaathiri Selous! Eti, itapunguza watalii.
Stiegler’s ikakwama! Sasa Stiegler’s inajengwa, lakini hadithi ni zile zile! Wanaojiita wanaharakati wa mazingira wanadai mradi huo utaathiri Selous, wanadai una gharama kubwa, wanadai kuna viumbe adimu Selous! Yaani chura, popo, vipepeo ni adimu na wana thamani kuliko Watanzania! (sikiliza mmoja wao)
Wakati Misri inakusudia kujenga Aswan, Israel akisaidiana na Marekani walikuja juu! Wakamsakama Gamal Abdul Nasser! Lakini, Farao akasimama wima ikajengwa. Akina Israel wakaja Afrika Mashariki kutuambia tukatae, maana watatumia maji yetu! Yani maji ya Ziwa Viktoria na Mto Nile! Wakatuhamasisha tujenge miradi mikubwa ya maji ili yanayoenda Misri yapungue!
Ukweli ni kwamba, maji ya Nile yanazidi mahitaji ya Tanzania, Uganda, Ethiopia, Sudan na Misri. Bado tunatumia chini ya 50% ya maji. Mengi yanaishia Bahari ya Mediterranean ambako hata Israel inanufaika nayo. (Kwa wasiojua maji ya Mto Nile siyo ya Ziwa Victoria). Hatimaye Nasser akapoteza maisha baada ya kushindwa vitani. Lakini, bwawa la Aswan lipo na ndio msingi wa Maendeleo ya Misri.
Bwawa la Akosombo nalo halikubaki salama. Ni moja ya mambo yaliyowaudhi Waingereza hadi wakasuka mapinduzi ya kumng'oa Kwame Nkurumah. Lakini, mwana wa Afrika alijenga bwawa hilo. Bwawa la Akosombo ndio kiini cha Maendeleo ya Ghana, linauza umeme Togo, Benin, Cameroon na Nigeria!
Cahora Bassa nalo halikumuacha Samora Machel salama! Likitumika kudhoofisha uchumi na harakati za ukombozi Msumbiji. Wakubwa walilipinga! Afrika Kusini ya makaburu ikawezeshwa kujenga vinu vya nyuklia ili bwawa likihujumiwa aumie msumbiji peke yake! Hao hao wakaja kuwanyang'anya vinu vya nyuklia ilipoonekana ANC itatwaa madaraka! Hawataki ngozi nyeusi imiliki nyuklia!
Bwawa la Blue Nile nalo lilipingwa mno! Lakini, Zenawi akafumba masikio. Linajengwa kwa kasi sasa kwa msaada wa China. Ethiopia inasonga mbele kwa kuwa imeongeza umeme. Sasa wana treni ya umeme.
Hata nia ya Uganda kujenga bwawa Jinja nayo ilipingwa!
Hii ndio historia ya mabwawa Afrika! Wakubwa hawataki tupate umeme. Wanajua umeme utazalisha Viwanda na tutatumia rasilimali zetu wenyewe. Bahati mbaya, Afrika haina uhaba wa vibaraka! Toka enzi za Lumumba, Nasser, Nkurumah! Mara zote na kote watajitokeza kuwaunga mkono mabeberu. Wanatumia sababu zile zile za enzi za akina Lumumba. Tuwapuuze! (Sikiliza Hayati Magufuli)
Watanzania tunaduwazwa na wanasiasa.Asante Mwengeso kwa mada hii.Kwa uongozi tulio-nao sasa na background yake(from NGOs) na main backer wao(Kikwete),sina shaka yeyote kwamba hii ni kweli.Time will tell,ilà mficha maradhi kifo humuumbua.Wataumbuka tu.
Nina sehem nyingi za kukosoa kwenye hiyo miradi ya umeme.Kwa kuwa wewe umefanya research, onesha uwongo na weka ukweli
Nina sehem nyingi za kukosoa kwenye hiyo miradi ya umeme.
Ukiuliza watu wawili - watatu unaweza futa post nzima.
Mkuu umejitahidi sana kuelezea kinagaubaga na kuambatisha vielelezo toka vyanzo mbali mbali katika thread yako hii,ili kututoa giza.JF ni jukwaa la majadiliano na kuelimishana. Hivyo basi toa maelezo kuhusu hili ulilosema kwamba: Nina sehem nyingi za kukosoa kwenye hiyo miradi ya umeme, ili post yangu ipuuzwe
Nile ya Jinja ilijengwaCahora Bassa (Msumbiji/Afrika Kusini) Aswan (Misri) Akosombo (Ghana), Blue Nile (Ethiopia), Mto Congo (DRC), Jinja (Uganda) na Stiegler’s Gorge (Tanzania).
Muandishi ni PhD kweli?? Hivi anajua maana ya bio diversity kweli? Hajui kwamba binadamu pia inategemea species tofauti ili tuweze kusurvive? Anafahamu mentallity ya binadamu ni bora kuliko ndege na wadudu ndio ilisababisha moja ya janga kubwa katika historia ya dunia?, wanadai kuna viumbe adimu Selous! Yaani chura, popo, vipepeo ni adimu na wana thamani kuliko Watanzania! (sikiliza mmoja wao)
Huyu PhD uchwara anapotosha tena, mradi gharama zake ni Trillion 180 Za Kitanzania hao DRC wangetoa wapi hela?Kwa kuzuia ujenzi wa bwawa lile, mabeberu walifanikiwa kuzuia maendeleo ya bara zima la Afrika, kwani kusingekuwa na kijiji au nyumba Afrika ingekosa umeme. Viwanda vingechomoza mpaka vijijini
Mradi uliachwa mwaka 1989 na makaburu wenyewe maana iliwakamua pesa nyingi sana sasa sijui ni lini walinyang'anywa na mabeberu. In fact serikali ya Makaburu ilikua imewekewa vikwazo na mataifa mengi tu ya mabeberu sasa sijui hyu PhD anataka kupotosha historia kwa faida ya nani.Afrika Kusini ya makaburu ikawezeshwa kujenga vinu vya nyuklia ili bwawa likihujumiwa aumie msumbiji peke yake! Hao hao wakaja kuwanyang'anya vinu vya nyuklia ilipoonekana ANC itatwaa madaraka! Hawataki ngozi nyeusi imiliki nyuklia!
Muandishi ni PhD kweli?? Hivi anajua maana ya bio diversity kweli? Hajui kwamba binadamu pia inategemea species tofauti ili tuweze kusurvive? Anafahamu mentallity ya binadamu ni bora kuliko ndege na wadudu ndio ilisababisha moja ya janga kubwa katika historia ya dunia?
Great Leap Forward 1958-62: Vita ya mwanadamu dhidi ya viumbe ilioua watu Million 50
Habari za sikukuu wana JF natumaini kila mtu ni mzima wa Afya bila kupoteza muda twende kwenye mada na ningeomba tuisome kwa umakini sana maana kuna jambo kubwa nataka tujifunze mwishoni, Karibuni. UTANGULIZI Tumeshazoea mara zote vita ni kati ya mataifa na mataifa au serikali na waasi n.k...www.jamiiforums.com
Inaweza kuwapo sababu bora zaidi za kupromote mradi huu ila sio kwa sababu eti vipepeo sio bora kuliko binadamu, very illogical argument.
Mama amenisikitisha sana mtu akiyeponda huo mradi ndo leo kakabiziwa asimamie mradi mbona kitukoSina imani na makamba hata kidogo, Kalemani angeweza kumaliza Ujenzi salama, Makuwadi wa mabeberu wanafanya kila jitihada kuturudisha nyuma, tutavuka MUNGU Mkubwa.
Bari = baliBari ni nini?