Kuna nini nyuma ujenzi wa bwawa la Nyerere la kufua umeme

Nakubaliana na wewe kuwa muandishi na hata baadhi yao humu wanadhania labda hii dunia ni kwa ajili ya binadamu tu. Hivi Mwenyezi Mungu kama alitaka binadamu tu wawepo hapa asingeumba na hao viumbe wengine. Kila kiumbe kina umuhimu wake katika dunia hii yetu, kwa hivyo tusijifanye eti sisi ni wajuaji wa kuamua kiumbe gani kiondolewe na kipi kibaki.

Muandishi kwa kweli anahitaji kupata elimu kubwa kuhusu bioanuwai.
 
Nimekuelewa sana mkuu kwa Uzi huu....

Bwawa la Stigla..... Kwa kweli sasa linahujumiwa...

Hata kumwondoa Kalemani kwenye sekta hii... Ni mkakati uleule ulioutaja hapo kwenye uzi.....
Wapigaji@work.
 
Kutawala sio kuwaharibia makazi yao, hta Biblia unayonakili kuna mahali inakataza ukataji wa miti inayosupport maisha yetu.

Deuteronomy 20:19
When you besiege a city for a long time, making war against it in order to take it, you shall not destroy its trees by wielding an axe against them. You may eat from them, but you shall not cut them down. Are the trees in the field human, that they should be besieged by you?

So kama hoja ni Biblia then mpka hapo mmeshatenda dhambi.

Anyway hoja yangu haikua kidini bali kibaiolojia kwamba huwezi toa argument kwamba Vipepeo au miti haina thamani kuliko binadamu unless hatujui jinsi food chain inavyofanya kazi.
 
Construction of the dam began on Nov. 6, 1956, and was completed in 1959
Shukrani mkuu kwa facts ulizomwaga. Maana kuna mentality kwamba kila failure ya waafrika ni hujuma ya wazungu. Sasa cha kujiuliza hizo Hydro power walizojenga kabla ya uhuru ilikua kwa ajili ya nani?
 
Mama yetu sijui hata kama huwa anapata muda wa kusoma vitu kama hivi au anasubiri ushauri wa Waziri wa Twita.
 
Huyu waziri wa Twita awe na huruma hata kidogo, anataka kutuletea umeme wa solar na Upepo ilimradi tu anufaishe tumbo lake.
 
Wanaomiliki gesi ni wazungu ndio wanaowauzia serikali umeme kwa bei juu unafikiri watakubali bwawa lijengwe?
 
Wanaomiliki gesi ni wazungu ndio wanaowauzia serikali umeme kwa bei juu unafikiri watakubali bwawa lijengwe?
Wanauza umeme?? Au wanauza gesi?? Na kama ulitaka wazungu wasimiliki vitalu na refinery wewe una hizo trillion 20+ za kumudu uwekezaji wa kuchimba gesi?

Then kwanini wapinge Bwawa lisijengwe ilihali 60% ya umeme wa TZ unatumia gesi tayari?? Yaani hta bila Bwawa la Nyerere tayari Gesi inadominate sekta ya nishati sasa kivp waje kuogopa umeme wa maji?
 
Huyu waziri wa Twita awe na huruma hata kidogo, anataka kutuletea umeme wa solar na Upepo ilimradi tu anufaishe tumbo lake.
Hilo lipo kwenye ilani ya CCM na mpango wa tatu wa maendeleo ya taifa. Yote yaliandikwa na JPM. In fact mpka umeme wa joto ardhi uliandikwa humo so mnamlaumu bure tu.
 
Kwahiyo hata SGR tusijenge kwasababu tu ina gharama kubwa kuliko MGR zilizopo? Angalienu ufanisi sio gharama pekee. Otherwise hta flyover msingejenga maana ni gharama kuliko barabara za chini!!
 
Blah blah. Ni mradi wa kipuuzi wa karne. Yani tuangalie metrics. Takataka kubwa linazalisha MW 2100 tu. Wakati gesi na upepo vinazalisha mara nyingi zaidi kwa gharama ndogo. Pia ni backward thinking za kishamba kutegemea maji karne hii ambayo kuna climate change. Maji ni unreliable. Kichwa kibovu tu kinachowaza miaka 60 nyuma ndio kinaweza kushabikia upumbavu kama huo. Yani kiufupi lile ni li swimming pool kubwa tu. Yani katiba yetu ingekuwa inawajibisha viongozi, angetapika kodi zetu. Nonsense.
 
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hizi nadharia za kusingizia mabeberu ndio kikwazo cha maendeleo yetu waafrika hazina nafasi kwa fikra za sasa.
Matatizo ya mwafrika yanasababishwa na mwafrika mwenyewe.
 
Kiburi ya china ni kuzalisha Umeme kwa bei ya chini sana na wa uhakika
 
Kuna kitabu kinaitwa Makuwadi wa soko huria kimeeleza kwa kina hujuma juu ya mradi wa rufiji
 
Mtoa Mada ameongea mambo ya ukweli. Hakuna beberu anayetaka azidiwe na nchi yoyote ya Africa. Wazungu wanataka daima Africa iwe chini yao. Haiingii akilini eti uharibifu wa mazingira upi? Hao nao ni mamluki wa mabeberu wasioitakia mema Africa. Anasimama mbunge na kutetea upuuzi hta hana haya. Yaani pori lote lile lina uwiano gani na hako ka bwawa? Hilo bwawa ni ndogo, ni kama shimo la mhanga kati Kati ya pori kubwa wala hakina madhara yoyote. Acheni hujuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…