Kuna njia ngapi za kufanya kesi, vigezo gani hutumika kupeleka kesi mahakama ya juu?

Simplicity.

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
2,636
Reaction score
1,662
Wakuu,

Najua hapa kuna watu waliobobea mambo ya sheria, hasa zile zinazohusiana na makosa ya jinai. Kuna wahalifu nimewashtaki mahakama ya mwanzo, sasa naona kila nikienda kesi inapigwa tu tarehe. Rushwa sitoi ng'o, hakimu asitegemee, tena hata ukaribu naye sitaki.

Sasa natafuta vigezo vya kuidisqualify mahakama hii ya mwanzo na mahakimu wake uchwara ili niende ya wilaya, huko kidogo nahisi mahakimu wana akili.

Kwanza naomba kujuzwa kuwa kuna namna ngapi za kufanya kesi mahakamani? Hapa naamanisha kuna njia zingine za kufanya kesi kama vile kwa simu, video conferencing (mfano kupitia skype, Gtalk, n.k), kwa kuwasilisha waraka wa maandishi au njia ipo moja tu kama tulivyoizoea ya mlalamikaji/walalamikaji na mtuhumiwa/watuhumiwa wote kuwepo mahakamani physically?

Pia naweza kutumia vigezo gani, kuhama kutoka mahakama ya mwanzo kwenda ya wilaya?
 
Wasamehe hao wahalifu wako kwanza ndio uje uombe ushauri
 
ujasaidia mkuu atasemee wangap?? katka dunia yaleo.kaka achana na mawazo ya kukatisha tamaaa kwa namna hii data njia sahh utasaidiwa
 
kwanza nianze na kukusahihisha kidogo katika kutumia lugha ya kisheria, hatusemi 'kufanya kesi' bali tunasema kuendesha kesi.

kesi inapokuwa mahakama ya mwanza na unataka kesi hiyo ikasikilizwe katika mahakama ya wilaya waweza fanya yafuatay
1. kukata rufaa kwa njia ya maomi rasmi mara baada ya kusomwa hukumu na wewe kutoridhika na maamuzi ya mahakama hiyo( katika hatua hii ni lazima kesi iwe imefika ukingoni)
2. kuangalia aina ya kosa, na kama kosa hilo unaona yafaa lisikilizwe na mahakama ya wilaya, basi pia waweza kuondoa shitaka hilo katika mahakama hiyo na kupeleka shauri lako katika mahakama ya wilaya
3. Ikiwa watatka kuwakilishwa na mwanasheria basi waweza peleka ombi hilo katika mahakama hiyo ili kesi hiyo ikasikilizwa katika mahakama ya wilaya kwa sababu wakili haruhusiwi kusimama katika mahakama ya mwanzao

kuhusu namna ambavyo wahusika katika kesi wanavyopaswa kutokea mahakamani
JIBU. hadi sasa basi njia ni ileile ya asili ya kuwataka wahusika wapande zote mbili watokee wenyewe au kwa kupitia mawakili wao. kwa maelezo hayo ifahamike kuwa, ushahidi kutolewa kwa njia ya kiiletroniki bado haujaanza kutumika lakini ushahidi wa kiiletroniki unakubarioa
 
kesi hii anasema ni ya jinai sasa yeye atakataje rufaa? Siyo jamhuri hapa? manake yeye ni shahidi tu katika shauri.

pili, kama nilisikia kwenye kesi ya Mahalu ulitolewa ushahidi wa teleconference, au sikusikia vizuri?
 
Wakuu,

Najua hapa kuna watu waliobobea mambo ya sheria, hasa zile zinazohusiana na makosa ya jinai. Kuna wahalifu nimewashtaki mahakama ya mwanzo, sasa naona kila nikienda kesi inapigwa tu tarehe. Rushwa sitoi ng'o, hakimu asitegemee, tena hata ukaribu naye sitaki.

Sasa natafuta vigezo vya kuidisqualify mahakama hii ya mwanzo na mahakimu wake uchwara ili niende ya wilaya, huko kidogo nahisi mahakimu wana akili.

Kwanza naomba kujuzwa kuwa kuna namna ngapi za kufanya kesi mahakamani? Hapa naamanisha kuna njia zingine za kufanya kesi kama vile kwa simu, video conferencing (mfano kupitia skype, Gtalk, n.k), kwa kuwasilisha waraka wa maandishi au njia ipo moja tu kama tulivyoizoea ya mlalamikaji/walalamikaji na mtuhumiwa/watuhumiwa wote kuwepo mahakamani physically?

Pia naweza kutumia vigezo gani, kuhama kutoka mahakama ya mwanzo kwenda ya wilaya?

Wewe mwenyewe si Mtatua matatizo sawa na ID yako ioneshavyo??? Am kidding bana, kwakweli sijui hizo procedure ila naamini utasaidiwa na wanasheria hapa.

Goodluck
 
Back
Top Bottom