Hii nchi ina vituko sana.
Kuna wageni kutoka marekani wametembelea Tanzania kujifunza mambo flani flani,boss wangu akaniteua mimi na wenzangu wawili tuwaongoze kwenye shughuli zao zilizowaleta.
Cha ajabu kuna office tumeenda leo,office nzima hakuna anayeweza kuongea kiingereza kizuri,hadi mkurugenzi wa office ni zero kwenye kiingereza, eti mkurugenzi akanivuta pembeni akaniambia hayuko vizuri kiafya hivyo anaomba anikabidhi kwa meneja wake ili atusaidie shida yetu,
Meneja nae akazuga eti yuko busy lkn baadae akanivuta pembeni akaniambia huwa anapata shida kuelewa accent ya kimarekani hivyo anaomba niwe namtafsria wanachoongea hawa wageni.
Nimeshangaa sana aisee.