Kuna pages huko Facebook zinauza pikipiki hadi 700,000 , 800,000 , 1,000,000 n.k hivi hizi ni nzima????

Kuna pages huko Facebook zinauza pikipiki hadi 700,000 , 800,000 , 1,000,000 n.k hivi hizi ni nzima????

Tanki

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
538
Reaction score
246
Unakuta picha ziko vizuri kabisa kiasi kwamba mtu hadi unajiuliza mbona kama muonekano na Bei haviendani. Unakuta chombo inauzwa 800,000, arafu muuzaji anasema chombo Ina documents zote. Na unakuta ni ofisi kabisa ya kuuza pikipiki used. Binafs mashaka yangu ni Bei zao.

Kwa wajuzi naomba kujua, hivi hizi pikipiki za Bei hizi ambazo ni used
650,000, 700,000, 800,000 , n.k je ziko poa kweli????
 
Ogopa kununua vitu used hapa bongo. Nunua tu pale unapokuwa na uhakika anayekuuzia ni mmiliki halali wa hiyo mali.

Kuna mali zingine za wizi.
 
Naomba kujuzwa wakuu,
kuna yule alichomwa moto hapo juzi jumapili saa4asubuhi, segerea akiwa amepaki kijiweni na wenzake kusubiria abiria, maskini ya Mungu sijui alinunua kiasi gani au alikua deiwaka tu, halafu ilikua imefungwa gprs kabisa na nadhani hakujua alifurahia bei chee 🐒
 
Back
Top Bottom