Kuna sadism inayopaswa kupigwa vita kwa kutumia nguvu zote ziwe za kimawazo au kivitendo.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Neno Sadism ni la lugha ya kingereza, kiswahili chake ni ukatili. Au mtu kufurahi anapoona mwingine anaumia.

Hii ni hulka mbaya sana, kwa maneno mengi kupenda kuona unyama ukiwatesa baadhi ya watu. Mtu anapoumia nafsini au mwilini ndipo mwingine anafurahi.

Miaka ya hivi karibuni sadism imeingia nchini mwetu kwa kasi ya ajabu. Unaamka asubuhi unakutana na habari ya mtoto wa miaka minne au saba kutekwa na wazazi wanaoomba habari isambazwe kadri iwezekanavyo.

Mtoto akibahatika kupatikana, Mama anasambaza sauti ya kurekodi kwa marafiki zake akimshukuru Mungu. Tujaribu kujiweka katika nafsi ya Mama au Baba wa mtoto wakati akiwa bado hajapatikana.

Hata kauli za baadhi ya viongozi ni kielelezo cha uwepo wa sadism. Sio spirit nzuri kuisambaza kwani wanaoumizwa ni wengi kuliko wachache ambao hawaumizwi.

Kama ni kupitia kwa mapadre na mashekhe basi na juhudi zifanyike katika kuliombea taifa liondokane na roho hii ya mtu kupenda kuona mwenzake akiumia ndipo furaha iwe sehemu ya maisha yake.
 
Hiyo sadism inatokea juu kuja chini....kama mtu anachukia tajiri bila sababu ya msingi, watu wa kikosa ajira kwa kutumbuliwa watu wanafurahi wanaona ni sifa.....
 
Mtetezi wa Jiwe leo umekuja kivingine tena kwa aibu huku ukijaribu ukizungukazunguka.

Ni wazi umeogopa kushushuliwa ndio maana umekwepa kusema directly lililo moyoni mwako kwa uliemlenga.

Mtakumbuka sana maneno ya Lissu.
Mtetezi wa jiwe kagusa maeneo mengi kwa wakati mmoja.
 
Mtetezi wa Jiwe leo umekuja kivingine tena kwa aibu huku ukijaribu ukizungukazunguka.

Ni wazi umeogopa kushushuliwa ndio maana umekwepa kusema directly lililo moyoni mwako kwa uliemlenga.

Mtakumbuka sana maneno ya Lissu.
mkuu anapo hubir ubaguzi kila siku anadhan anajenga kumbe anabomoa? duniani pote hakuna asiyepingwa
 
Mtetezi wa Jiwe leo umekuja kinamna nyingine kabisa..
Lijamaa lenu ndio limeleta chuki miongoni mwa watanzania na kuiharibu Nchi..
Madhila yote haya ya watu kupigwa risasi, kutekwa, nk yameanza awamu hii..
Funguka ndugu.
Usisahau ya Dr Ulimboka na Absalum Kibanda, japo hawa ni wahanga wa kutekwa kiteswa na kutoswa kusikojulikana kwa awamu ya 4. Ya awamu hii yanatisha zaidi!
 
Mtetezi wa Jiwe leo umekuja kivingine tena kwa aibu huku ukijaribu kuzungukazunguka.

Ni wazi umeogopa kushushuliwa ndio maana umekwepa kusema directly lililo moyoni mwako kwa uliemlenga.

Mtakumbuka sana maneno ya Lissu.
amekosa U DC
 
Mwingine tena kapigwa visu mpaka kafa kisa ni vitz tu!!. Usalama wa taifa pale pembeni ya Saint Peters watu wanalipwa pesa nzuri tu kila mwezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…