Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Neno Sadism ni la lugha ya kingereza, kiswahili chake ni ukatili. Au mtu kufurahi anapoona mwingine anaumia.
Hii ni hulka mbaya sana, kwa maneno mengi kupenda kuona unyama ukiwatesa baadhi ya watu. Mtu anapoumia nafsini au mwilini ndipo mwingine anafurahi.
Miaka ya hivi karibuni sadism imeingia nchini mwetu kwa kasi ya ajabu. Unaamka asubuhi unakutana na habari ya mtoto wa miaka minne au saba kutekwa na wazazi wanaoomba habari isambazwe kadri iwezekanavyo.
Mtoto akibahatika kupatikana, Mama anasambaza sauti ya kurekodi kwa marafiki zake akimshukuru Mungu. Tujaribu kujiweka katika nafsi ya Mama au Baba wa mtoto wakati akiwa bado hajapatikana.
Hata kauli za baadhi ya viongozi ni kielelezo cha uwepo wa sadism. Sio spirit nzuri kuisambaza kwani wanaoumizwa ni wengi kuliko wachache ambao hawaumizwi.
Kama ni kupitia kwa mapadre na mashekhe basi na juhudi zifanyike katika kuliombea taifa liondokane na roho hii ya mtu kupenda kuona mwenzake akiumia ndipo furaha iwe sehemu ya maisha yake.