Kuna shida gani Tanzania ikitangaza rasmi kuisaidia Congo kupambana na M23? Tuna Viongozi wa namna gani?

Kuna shida gani Tanzania ikitangaza rasmi kuisaidia Congo kupambana na M23? Tuna Viongozi wa namna gani?

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Leo tunajenga reli ya SGR kwa dhumuni ifike Mashariki mwa Congo. Swali ni Je hiyo reli itakuwa na faida kama Mashariki mwa Congo kukiendelea kuwa vitani namna hii?

Tuache suala la reli. Hivi Je Viongozi wetu hawajui tunaweza faidika kiuchumi endapo leo hii tukiwasaidia wazi Congo kwenye vita yao dhidi ya M23?

Marekani, Uingereza na Ujerumani wanatoa msaada mkubwa kwa Ukraine kupambana na Urusi. Msaada ule sio msaada kama msaada ni mkopo ambao Ukraine watazilipa nchi zile kwa miaka mingi ijayo!

Tuseme Viongozi wetu hawa hawaoni kuwa tunaweza kutoa msaada wa kijeshi kwa Congo sisi kama Tanzania ( Sio chini ya mwamvuli wa SADC au AU au EAC) na tukautumia kama mkopo kwa nchi ya Congo ambapo baadae watatulipa hata kwa karne nzima na tukafaidika kiuchumi?

Hivi nchi hii kuna Think Tanks? Ni kina nani hao Think Tanks? Wana Mchango gani positively kwa maendeleo ya Taifa?
FB_IMG_1738072479479.jpg
 
So kwa hoja yake una maanisha Rwanda kashindikana? Na anaweza fanya lolote lile bila kufanywa chochote kile?
Hapana. Katika geopolitics kuna vitu vingine unafanya kimya kimya. Rwanda anajua kabisa JWTZ wakienda kusaidia DRC dhidi ya M23 ni kwamba wanapigana dhidi ya wanajeshi wa Rwanda. Sasa badala ya kupiga kelele tunafanya kimya kimya tu.Kumbuka hata Rwanda anasema yeye majeshi yake hayapo DRC na M23. Kwa hiyo acha zipigwe kimya kimya. Tatizo ni kwamba Kagame anaona jeshi lake ni kiboko sana hakuna nchi ya Africa inaweza kumpiga
 
Unadhani nafasi ya Tanzania kwenye maamuzi na uchumi wa Congo itakuwaje endapo Tanzania ikitangaza wazi kuisaidia Congo na kushusha vikosi vyake waziwazi pale Congo?
 
Tatizo lipo kati ya Rwanda, DRC na M23, kwa nini tujiingize kwenye mgogoro mkubwa tusiouelewa hata kidogo?!
Hatuuelewi mgogoro kivipi?

Kwa hiyo wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania waliopo kule Tabora na Katavi wakisema Tabora na Katavi ni mali yao tuwaache tu?

Unafikiri kwa kutumia nini?
 
Back
Top Bottom