Kuna shida mahali!

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Habari zenu ndugu wana JamiiForums, nimeona kama kawaida yangu na hili niwashirikishe kuna ndugu wa karibu mwenye jinsia ya kike umri wake kwa sasa anaweza kufikia miaka 52 amekuwa na tabia ambayo kidogo inanichanganya.

(1) Akikuta naongea na mwanamke kwa mahaba uso wake unabadirika na kuonyesha chuki kuu yaani hapendi kabisa hiyo hali.

(2 ) Vitu vyangu vya samani huvifanyia fujo yaani hajali kuwa vinaweza kuharibika mfano masofa na gesi.

(3 ) Nikienda kumtembelea kwake hupenda kunisachi kwenye begi langu na kama akikuta condom au sigara huvichukua ( sielewi kuwa huwa anaenda kuvitupa au anaenda kutumia!)..

(4) Anajisikia amani sana akiniona naishi maisha ya kisela yaani nisiwe kabisa na mpango wa kuanzisha familia. Wakuu nahitaji maoni yenu na mchango wenu
 
Mkuu, aliwahi kukuchagulia mwanamke wa kuoa ukamkataa?
 
Ndugu damu damu au mtoto waba mkubwa na mdogo...?🤣🤣
 
Na wewe 30+ kwann usiwe na strong relationship???
Mwenzio anaona kama mnawezanaa, ndy maana anakufanyia visa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…