Sisi Wakristo sio wajinga kama unavyodhani,ni kweli tupo upande wa Israel hata kama wao wengi sio Wakristo,yote hayo sisi tunayatambua kwani bila wao kumkataq Yesu na wokovu sisi leo tusingepata neema hii ya wokovu ni kweli kwasasa hawamtambui Yesu kama mwokozi(masihi)wao ila haya yote yalishaongelewa kwenye biblia kwani siku sio nyingi watatubu na kupokea neema ya wokovu tena.
9 Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana na Yerusalemu.
Zekaria 12:9
10 Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
Zekaria 12:10
Katulie usome wayahudi watashituka kumwona Yesu waliemchoma watashangaa kuona walimsulubisha masiha wao nao wataombeleza na kutubu,wakati huo mataifa yatakuwa yamekusanyika Israel yatauliwa na masihi na mizoga yao kutapakaa.Israel ni saa ya dunia, Israel ni chanzo cha baraka yote duniani tutaendelea kujiungamaniusha nae mpaka mwisho wa dahari,uishi milele ee Israel wabarikiwe wakupendao na wanaokuchukia wawe adui za Mungu.