Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Wakati Shule zikiwa zinafungwa kwa kumaliza mwaka wa masomo lakini kuna baadhi ya Shule za msingi zinaratibu utaratibu wa Wanafunzi kutokwenda likizo badala yake wanashinikiza kuendelea na masomo katika utaratibu rasmi.
Mfano katika Shule ya Msingi Ndumbwi, iliyoko Mbezi Juu Jijini Dar es Salaam na Shule ya Msingi Africana iliyopo Salasala Watoto wa darasa la tatu ambao inaelezwa kwamba watahitimu masomo yao ya elimu ya msingi kwa kuishia darasa la sita wameambiwa ni lazima kuendelea kuhudhuria shuleni kama kawaida.
Hoja ambayo inaelezwa na Shule ni kwamba wanajitahidi kukimbizana na masomo ambayo wangetakiwa kuyasoma kufikia darasa la saba ili wawe wameyasoma yote wakija kuhitimu kwa kuishia darasa la sita.
Ilielezwa hivyohivyo kwenye likizo ya muhula uliopita Wanafunzi wakaendelea na masomo kama kawaida huku baadhi ambao hawakudhuria wakipewa adhabu.
Jambo la kushangaza Wanafunzi wanaelezwa ni lazima kwa kuwa mambo wanayofundishwa hayatarudiwa Shule zitakapofunguliwa, badala yake wanasema wataendeleza pale walipoishia kwa maana kwamba mambo yatakayofundishwa kipindi cha likizo yatahesabika kwenye utaratibu rasmi.
Licha hoja hizo lakini Wanafunzi wanatakiwa kuchangia Shilingi 500 kila siku kwa ajili ya kuwezesha masomo hayo. Jambo hilo linafanya wengi kujiuliza maswali bila majawabu rasmi na kuibua minongono.
Kama suala hilo linafanyika kwa msukumo wa hoja zilizopo hasa kukimbizana na utaratibu mpya wa kuhitimu elimu ya msingi, kwanini uathiri haki ya Wanafunzi kupata likizo kama taratibu zinavyoelekeza au utaratibu huo mpya umekuja na mabadiliko?
Kuwashinikiza Wanafunzi kwamba ni lazima kuendelea na masomo kwa kuwa hawatarudi nyuma kuwafundisha mambo ambayo watakuwa wamefundisha kipindi cha likizo ni kuwanyima haki yao muhimu.
Kama ni utaratibu rasmi wa kimasomo kama inavyodaiwa, kwanini Wanafunzi watozwe pesa za kila siku kuwezesha masomo hayo?
Sidhani kama Wazazi hawapendi Watoto wao wapate elimu, lakini sio sawa kuweka mazingira ya shinikizo ambayo ni kinyume na taratibu na yanayoweza kuathiri Wanafunzi, kuna wakati Wanafunzi wanahitaji kupata likizo ili kupata utulivu kwa kupumzika, kupata nishati mpya na hata kukaa na familia kushiriki stadi za maisha.
Wito wangu kwa mamlaka, ni vyema wakatoa maelekezo na msisitizo kwa Shule ambazo zinafanya hivyo au zinakusudia kufanya hivyo kuzingatia taratibu na miongozo bila kuathiri haki za Wanafunzi. Suala hili linafanyika katika Shule nyingi za Serikali hususani zilizopo Jijini Dar es Salaam.