DOKEZO Kuna Shule Wanafunzi wanashinikizwa wasiende likizo ili Walimu wakusanye michango, Mamlaka husika toeni mwongozo

DOKEZO Kuna Shule Wanafunzi wanashinikizwa wasiende likizo ili Walimu wakusanye michango, Mamlaka husika toeni mwongozo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Huu upuuzi nilishaukataa kitambo sana. Mkuu wa shule hawezi kunibakisha shuleni hata siku moja wakati ni likizo ya wanafunzi waende wakapumzike wajiandae na muhula mpya wa masomo. Kufundisha sana kutaka sifa ni ujinga unachosha wanafunzi
Mtumishi
 
Eti unakuta darasa la tatu na la sita hawafungi, haohao wakiingia la nne na la saba mwakani hawatafunga likizo zote ni kufululiza kufundisha tu mpaka kunako mitihani ya taifa. Huu mtindo ni wa kipuuzi na haupo katika kanuni za ufundishaji
Dunia uwanja wa kazi sio kupumzika aiseee
 
Elimu ni gharama weka pesa upate pesa weka muda upate mafanikio

Mwanao unaweza mchukua tu uondoke naye Kama yupo vizuri

Ila mtu Kama Mimi ambaye sipendi usumbufu akae uko atakuja kula xmass na mwaka mpya !!
Kugharimia elimu ya msingi ni upumbavu, gharimia elimu ya ufundi.
 
Walimu nao waneona wale kwa urefu wa kamba yao. Huu ujinga ulianza shule za biashara, watu wa serikali wakanogewa, na una back up ya watu wa wilayani kwa kuwa kuna 'mgao wao'.

Wale watetezi wa haki za watoto hutowasikia hapa - kwao kupumzika na kujifunza stadi za maisha si haki - kwao haki ni kutochapwa tu.

Watoto wanashindishwa shule kuliko wasomi wanavyoshinda maabara, na wakihitimu ili hali hawana stadi za mtaani wanaambiwa kwa kebehi 'jiajiri', ili hali muda wote alikuwa anakokotoa X.

Hizo shule wanasoma maskini kama wa Namtumbo - watoto wanaolelewa na wazee, watoto wa wauza maandazi, n.k ili hali wapo mitaa yenye ahueni kiuchumi.
Hizo jero jero ndo kuwa na mgao toka shuleni mpaka wilayani? Umasikini utazidi kulikumba hili taifa kwa mawazo haya au kwa vitendo hvyo. Jero jero za kila siku ndo zininnyime mwl uhuru wa kuwa likizo??
 
Back
Top Bottom