Mh Waziri wa Ardhi tupia jicho lako katika Wilaya ya Simanjiro kwani kuna dalili zote kuwa kuna siasa imeingizwa kwenye utengaji wa eneo la kilimo na ufugaji.
Suala la kutenga eneo la ufugaji na kilimo ili kuondoa migogoro baina ya wakulima na wafugaji lakini kuna watendaji wasio na maadili wanalitumia vibaya wazo hilo la Serikali.
Ndio maana kuna swali hili kuwa; je kuna Siasa katika kutenga eneo la kilimo na ufugaji ktk Wilaya ya Simanjiro?
Wadau mfikishe suala hili kwa wahusika ili walimulike na kulipatia ufumbuzi.