themagnificient
JF-Expert Member
- Dec 13, 2016
- 1,033
- 3,720
Hii nchi kuna matukio ambayo huwa yanaonyesha kabisa dalili kuwa kuna harufu ya maafa lakini Serikali huwa ipo kimya, ila likishatokea hilo tukio utashangaa yanatengwa mamilioni ya posho kwa ajili ya tume ya uchunguzi yani huwa wapo chap kuunda tume kuliko kupambana na majanga.
Pale kigamboni mimi sio mwenyeji ila nilishawahi kusikia wenyeji wa pale wakipiga sana kelele Mitandaoni wakimshinikiza Rais achukue hatua kuboresha vile vivuko au kuleta vipya kabisa ila nimeona bado Serikali ipo kimya.
Sasa juzi nikavuka kuelekea upande wa kigamboni kwa mara ya kwanza nikashtukia tukio ambalo watu niliwahi kuskia wanalalamika, Kivuko kilipofika kule upande wa Kigamboni kikashindwa kusimama eneo la watu wanaposhuka, nikashangaa kimezungushwa alafu ule upande wa tulioingilia ndio ukafanikiwa kutia nanga, Magari yakatoka kwa Rivas na hilo nimeshuhudia mimi mgeni ila wenyeji wana Mengi wanasema la juzi ni Chamtoto.
Rais Samia Suluhu Hassan Tafadhali angalia pale kwa makini, msisubirie siku watu wamwagwe pale mje na Habari za kuunda tume vile Vivuko vimechoka na sasa naona vinasubiriwa vilete majanga ndio mchukue hatua.
Mkiona hamuwezi kuendesha mleteni muwekezaji awe wa nje au mzawa ashushe vyombo vya maana pale kwenye kila 200 serikali ikate kodi yake au kama hamtaki kumpa mwekezaji Nunueni vivuko vipya hata mkichaji 300 ila watu wawe salama.
Kama tumeweza kununua Ndege mpya hatushindwi kunumua vivuko vipya pale.