DOKEZO Kuna siku pale Kivukoni yatatokea maafa, msikimbilie kuunda tume

DOKEZO Kuna siku pale Kivukoni yatatokea maafa, msikimbilie kuunda tume

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Zike boti ni hatari zaidi kuliko unafikiri. Pale upande wa kigamboni kuna mkondo wa maji una nguvu sana hasa wakati wa kupwa na kijaa maji. Kanageuka juu chini kale.
hii chai imezidi chumvi tena
 
In fact madude ni mabovu ila ukisema utaletewa nongwa.

Lile moja lilishawahi kupeperukia kule kama unaenda chuo cha Mwl Nyerere, cant imagine ingekuwaje kama liengepeperukia upande ule outer to the ocean kule sijui tungelikuta Reunion au Madagascar
Tugs zingeizuia lisiende huko
 
tumpe makhesa jaman sisi kama hatuwezi atuletee vyuma vya kisasa...
 
Nashukuru kwa taarifa! Nadhani kwa wale waoga wangetumia daraja la Kigamboni kuvuka.
 
Ndo tupo tunasukumizana kuingia kwenye sea taxi
IMG_20230104_173456.jpg
 
mtoa mada ni mgeni na vivuko, kivuko kugeuza upande wa pili
na kutoka kwa rivasi sio kuwa kivuko kibovu ilikuwa mlango umekataa kushuka hilo tu mlango haisababishi ajali yoyote, hizo zooote ni mbinu ya kutaka kumpa bakharesa hiyo sehemu.
 
Watu wa dar waoga sana, je siku mkishuhud1qia ya vivuko vya pangani, rufiji pale utete pia kile kuwa pale kilombero, vya kigamboni ni vya kisasa na smooth sana, bahari imetulia usisahau mto huwa una flow kwenda upande mmoja
 
Acha hizo ... Unataka kubania watu kwenye kuunda Tume ya uchunguzi. Huwa zinalipa sana kwa muda mfupi tu. Acha nongwa wewe panda ukifika salama shukuru shika hamsini zako. Mambo ya Ngoswe huwezi kujua. Nakushauri acha roho ya wivu kwa watu ambao watakuja husika kuunda Tume.
 
Leo 18.04.2023 saa 1.45 usiku Kivuko cha Sea Taxi kilizusha Taaruki kwa Abiria waliokuwa wakivushwa kuelekea Kigamboni, baada ya kukigonga Kivuko cha M.V Kazi Mita chache kabla ya kufika kwenye Gati. Taaruki ilikuwa kubwa, Shukurani kwa Mabaharia ya Kivuko kwani waliweza kutuliza Taaruki kwa kuwaomba watulie. Sikuweza kujua ilikuwaje mpaka kutokea Kivuko kuweza kugonga,lakini kuna Uzembe kati ya Manahodha wa moja ya Vivuko hivi. Jambo la kushukuru tulifika salama bila ya kuwepo Madhala yoyote.
 
In fact madude ni mabovu ila ukisema utaletewa nongwa.

Lile moja lilishawahi kupeperukia kule kama unaenda chuo cha Mwl Nyerere, cant imagine ingekuwaje kama liengepeperukia upande ule outer to the ocean kule sijui tungelikuta Reunion au Madagascar

[emoji23][emoji1787]dah
 
Back
Top Bottom