Kuna simu zinaitwa Aquous je zina ubora?

Kuna simu zinaitwa Aquous je zina ubora?

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
1718825597107.png

Kuna simu zinaitwa AQUOS mnaotumia humu zipoje? Ubora jee?

Maana nazo zinakuja kwa kasi nchini!!

Mnaozifahamu tafadhali mtujuze
 
Ni nzuri ukinunua kubwa zenye uwezo mkubwa, zipo mpaka za 5g lakini shida hazina spear na usije kusahau password utajuta kununua hiyo simu, maana hutoweza kuitumia Tena maana hakuna fundi anaeweza kuzitoa password hapa Tanzania
 
Fundi wa kuzitoa password wapo ila ni gharama kati ya 70k_- 150k. Kuhusu spea uko sahihi huku zinakuja za mtumba haziji mpya. Siyo aquos tu simu nyingi za Japan kutoa password ni mtihani.

Pia upande wa matumizi kuna mapungufu utayaona kwani ile simu imelengwa kutumika Japan pekee.
 
Mchina akishika soko hataki kulipoteza mtapigwa matoleo mtachoka wenyewe mfano mzuri kwenye simu na malori check Sinotruck anavyofyatua matoleo mapya kila siku ya Howo
Wabongo kwa kukaririsha kila kitu Mchina, AQUOS ni simu zinazotengenezwa Japan na ni kwa ajiliya Japan pekee huku bongo nyingi zinakuja mtumba na refurbished.
Nimetumia simu za Japan docomo ikiwemo LG, Sony kiufupi ni simu kali ngumu na nzuri zinadumu haswa, mapungufu tu ni pale unapotaka software update zinataka utumie network yao docomo.
Ukija kwenye AQUOS sasa kuna RT series bei ya RT7 ni kama iPhone macho matatu
 
Ni simu nzuri pia... Japo nyingi ni refurbished na refurb ni refurb tu haijalishi kutoka kampuni gani inaweza ikawa na vipengele ila ukipata nzuri utakaa nayo.

Binafsi natumia r6, sio mbaya sana kwa matumizi yangu hainikwazi. Nimetoa apps zote za kijapan nimeweka za gugo, nimeweka na gcam mtu anaweza sema ni pixel.

Iko nyepesi sana, processor yake ina nguvu japo ni disappointment kama wewe ni heavy gamer/user inapata sana joto hasa kama upo mazingira yenye joto. Na hii ni flagship nyingi zilizotoka 2021 ambazo zilikuwa equipped na sd888.

Kwenye kukaa na chaji hapa itategemea na matumizi yako tu (assume battery health iko njema), yakiwa heavy basi battery ita drain fast. Marafiki zangu naoshinda nao wanatumia flagships za samsung na iphone naona hatujapishana nao sana tena wao ndio wanaongoza kwa kujazia jazia chaji binafsi hata charger sikuhizi sitembei nayo.

Ila kwa matumizi yangu ya kawaida kupiga/kupokea simu, kuperuzi mtandaoni na kucheza games zangu ndogo ndogo iko poa sana. Nikilichaji mpaka 88% nina uhakika wa kurudi geto tambo bado lina chaji bila kuchaji hapo katikati.

Kitu sijapenda ni kwamba haipati latest Android version 14. Na pia design yake ya camera ya nyuma inaweza isikupendeze. Pia hautakuwa unajulikana unatumia simu gani kama watumiaji wengine wa samsung na iPhone. Mara nyingi mtu akishika simu yangu anauliza hiyo samsung/pixel/simu gani!

Yote ya yote ni simu nzuri kwa mtu asiye na mambo mengi au wale wazee wakupenda flagship specs kwa bei kitonga!

Cc Chief-Mkwawa karibu utoe neno.
 
Wabongo kwa kukaririsha kila kitu Mchina, AQUOS ni simu zinazotengenezwa Japan na ni kwa ajiliya Japan pekee huku bongo nyingi zinakuja mtumba na refurbished.
Nimetumia simu za Japan docomo ikiwemo LG, Sony kiufupi ni simu kali ngumu na nzuri zinadumu haswa, mapungufu tu ni pale unapotaka software update zinataka utumie network yao docomo.
Ukija kwenye AQUOS sasa kuna RT series bei ya RT7 ni kama iPhone macho matatu
Sony gani ulitumia?
 
Back
Top Bottom