Ni simu nzuri pia... Japo nyingi ni refurbished na refurb ni refurb tu haijalishi kutoka kampuni gani inaweza ikawa na vipengele ila ukipata nzuri utakaa nayo.
Binafsi natumia r6, sio mbaya sana kwa matumizi yangu hainikwazi. Nimetoa apps zote za kijapan nimeweka za gugo, nimeweka na gcam mtu anaweza sema ni pixel.
Iko nyepesi sana, processor yake ina nguvu japo ni disappointment kama wewe ni heavy gamer/user inapata sana joto hasa kama upo mazingira yenye joto. Na hii ni flagship nyingi zilizotoka 2021 ambazo zilikuwa equipped na sd888.
Kwenye kukaa na chaji hapa itategemea na matumizi yako tu (assume battery health iko njema), yakiwa heavy basi battery ita drain fast. Marafiki zangu naoshinda nao wanatumia flagships za samsung na iphone naona hatujapishana nao sana tena wao ndio wanaongoza kwa kujazia jazia chaji binafsi hata charger sikuhizi sitembei nayo.
Ila kwa matumizi yangu ya kawaida kupiga/kupokea simu, kuperuzi mtandaoni na kucheza games zangu ndogo ndogo iko poa sana. Nikilichaji mpaka 88% nina uhakika wa kurudi geto tambo bado lina chaji bila kuchaji hapo katikati.
Kitu sijapenda ni kwamba haipati latest Android version 14. Na pia design yake ya camera ya nyuma inaweza isikupendeze. Pia hautakuwa unajulikana unatumia simu gani kama watumiaji wengine wa samsung na iPhone. Mara nyingi mtu akishika simu yangu anauliza hiyo samsung/pixel/simu gani!
Yote ya yote ni simu nzuri kwa mtu asiye na mambo mengi au wale wazee wakupenda flagship specs kwa bei kitonga!
Cc
Chief-Mkwawa karibu utoe neno.