Kuna siri gani, chanzo cha kifo cha mzee John Kombe, watoto wake wataka taarifa za kifo cha baba yao zifutwe kwenye vyombo vya habari

Kuna siri gani, chanzo cha kifo cha mzee John Kombe, watoto wake wataka taarifa za kifo cha baba yao zifutwe kwenye vyombo vya habari

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Ikiwa ni zaidi ya siku 20 zimepita tangu mwili wa mzee aitwae John Kombe (73) mkazi wa kata ya Kirua Vunjo Magharibi mkoani Kilimanjaro, kudaiwa ulikutwa umefungiwa kwenye dula lake na watu wasiojulikana huku ukiwa majeraha, Jeshi la polisi mkoani humo limesema bado linaendelea na uchunguzi, na mwenye kujua siri ya tukio hilo atoe ushirikiano kwa jeshi hilo.

"Tunaendelea na uchunguzi wa kujua chanzo cha kifo chake kilisababishwa na nini, uchunguzi ukikamilika tutatoa taarifa kamili, na yeyote mwenye taarifa halisi ya tukio aje kwangu" Ujumbe mfupi uliotumwa kwa mwandishi wetu na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa.

Aidha, wakati huo huo kifo hicho kikiwa kimetawaliwa na usiri mzito isijulikane watu waliotenda tukio hilo, watoto wawili wakiume mzee huyo wamepiga simu kwa mwandishi wetu wakitaka taarifa zilizochapishwa kuhusu kifo cha baba yao zifutwe pasina kusema sababu.

"Unatafuta ugomvi ambao hautauweza, nina uhakika hiyo taarifa itafutwa, itatumika kila mbinu" Kauli ya kijana wa mzee huyo akizungumza na mwandishi wetu kwenye simu.

Ikumbukwe kuwa Novemba 30, 2025, mwenyekiti wa kitongoji cha Tela Kati katika kata hiyo aitwae Agust Kesi alizungumza na mwandishi wetu nakusema baada jeshi la polisi kufika na kuvunja mlango wa duka hilo walishuhudia mwili wa mzee huyo ukiwa na majeraha huku damu zikiwa zinatoka masikioni, puani na mdomoni.

Kuna siri.png
 
Back
Top Bottom