Kuna siri gani katika vijiwe vya kahawa kwa viongozi wa CCM?

Desprospero

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
1,015
Reaction score
2,493
Kuna mambo ukiona yanajirudia ni vizuri kujiuliza ili kujifunza. Wana JF tusaidiane.

Enzi za uhai wake tulimwona Hayati John Pombe Magufuli akinywa kahawa na vijana wake huko Chato. Hivi majuzi akiwa ziarani Singida tukaoneshwa picha Rais Samia Suluhu Hassan naye akiwa na kina mama katika kijiwe cha kahawa lakini yeye hakuonekana akinywa wala kina mama wale.

Swahiba wa Magufuli Paul Makonda naye baada ya kuteuliwa kuwa MC wa CCM naye huko Dodoma kaibukia kijiwe cha kahawa akiwa na baadhi ya wanachama wenzake wakiigiza kunywa kahawa.

Nini kilichojificha nyuma ya kahawa? Wanataka ku-win kitu gani? Huku siyo kuwahadaa vijana hawa?

Nini maoni yako!?
 
Caffein mkuuu unaambiwa kikombe kimoja cha kahawa sawasawa na soda za energy tatu
 
Kuna mambo ukiona yanajirudia ni vizuri kujiuliza ili kujifunza. Wana JF tusaidiane.

Enzi za uhai wake tulimwona Hayati John Pombe Magufuli akinywa kahawa na vijana wake huko Chato. Hivi majuzi akiwa ziarani Singida tukaoneshwa picha Rais Samia Suluhu Hassan naye akiwa na kina mama katika kijiwe cha kahawa lakini yeye hakuonekana akinywa wala kina mama wale.

Swahiba wa Magufuli Paul Makonda naye baada ya kuteuliwa kuwa MC wa CCM naye huko Dodoma kaibukia kijiwe cha kahawa akiwa na baadhi ya wanachama wenzake wakiigiza kunywa kahawa.

Nini kilichojificha nyuma ya kahawa? Wanataka ku-win kitu gani? Huku siyo kuwahadaa vijana hawa?

Nini maoni yako!?
Kucheza na akili za wajinga ili waonekane ni watu wa chini ilhali ni mafisadi wa kutisha
 
Back
Top Bottom