Kuna Siri Gani Kwenye Kiapo cha Upadre!

Kuna Siri Gani Kwenye Kiapo cha Upadre!

Kusema hawako sawa kiakili si kweli, padri kalugendo yule wa bukoba yuko sawa tena sana, dk slaa yuko sana, father nkwera yuko poa...sijui unaowajua wewe lakini si kwasababu ya kuacha upadri....hata hivyo kuacha upadiri bado kuna nadhiri unaingia za kutunza siri za kanisa
Na iko siku, ikifika watarudi kutubu, kuna mmoja kwa macho yangu tumemkuta tena mie sikuwa najua kama alikuwa, ss alipotaka kurudi sindiyo tukajua tena mwanaye tulikuwa tunasoma wote nikauliza kwa baba akasema ndiyo kurudi ndani ya mwaka akarudisha majeshi
 
Mkuu umeelezea vizuri sana ila hapo kwenye kipengele cha kulala kifudifudi na kusomwa Novena kuna kitu kikubwa zaidi ya hicho.jibu lake hapa haliwezi kupatikana labda aje mmoja alieishia ktk nafasi hiyo atueleze,japo nao kueleza ukaelewa huwa wanashindwa maana hili ni fumbo au tuseme ni jambo la ki-Mungu zaidi.
Novena maana yake ni TISA! ya kusali siku tisa katika Ukatoliki kuna aina za sala ambazo mtu kama anataka omba kitu basi atasali siku tisa mfululizo bila kuacha siku moja kuomba na muda mwingine uambatana na kufunga siku zote tisa....ujui nini unachoongea.
Kama Mkatoliki nakueleza kile nilichoishi na vile nilivyojifunza na kuona.unangangania fumbo fumbo....wakati ata maana ya neno Novena ulijui maana yake. Wakatoliki wana Ibada nyingi .kuna ibada ya ndoa,upadre,ibada ya kuombea marehemu,Ibada ya ubatizo n.k Hivyo basi nakushauri usome ,soma tena soma aipendezi kuongea na kushabikia kitu usichokijua kiundani
 
Balozi Dr. Slaa unahitajika huku haraka.
Kwanza tufahamu kuwa yaliyotokea na yanayotokea hayana budi kutokea na hakuna mwenye uwezo wa kuyazuia yasitokee.
Pili yote anayoyafanya Kwasasa Slaa hana hiari nayo si kwa maana ya ccm au wale wanaomfadhili kwa sasa bali ni laana ya kiapo na nadhiri zake...hawa wanaomfadhili ni kiambishi tu cha nguvu iliyo nje ya uwezo wa kibinadamu .
Slaa anateswa na haiba na kiapo, nadhiri na ahadi ya kutumikia kiapo.. Nimekutana na viapo Nimeishi maisha ya viapo lakini SIKUAPA. viapo ni vibaya na viapo havifi na kuviuwa kunahitaji mlolongo mrefu na wenye mambo mengi.
Slaa Aliitwa kwa wito kuonyesha na kutumia vipawa vyake kwa njia ya upadri akakubali na kupokea mpaka daraja la upadirisho mbele ya mimbari takatifu...aliingia mkataba na Mungu na kukamilisha wito.
Bahati mbaya sana akakengeuka nakuanguka moja kwa moja na tangu hapo viapo nadhiri na laana vikaanza kumuandama.
Siasa sio dini siasa ni propaganda siasa ni unafiki siasa haina kweli na Siasa haiongozwi na roho mtakatifu.
Kwa laana ile ya kiapo na nadhiri akajikuta anaangukia kwenye Ulimwengu wa mapepo na roho za kutangatanga.. Na tangu hapo ameendelea kutangatanga kuanzia kwenye mahusiano mpaka kwenye maisha.
Hakuna ambacho ameweza kufanya kikakamilika, amekosa ndoa takatifu amekosa maisha ya kudumu Kwenye siasa amekosa Kuacha Heshima na historia ya kutukuka kwenye lolote alilolifanya.
Kila alipoanza alianza vizuri kwa mafanikio na kupendwa sana lakini mwishoni kila kitu kikaenda kombo na kugeuka ubatili.... Kiapo kinamtesa.. Na haya ndio atakuwa maisha yake mpaka kaburini .
Viapo ni vibaya hakikisha unatengua kama hutaki kuendelea nacho viapo vina roho na roho haifi, mengi mabaya yatamtokea Dr na hii ni kanuni ya kidunia katika Ulimwengu wa roho.

Hii ni kutokana na maandishi ya Mshana Jr. wa jukwaa la wachawi.
 
Hivi mkuu pale panakuwaga na mkeka kweli!? Navyojua mimi ile ni ibada ya kuwekwa wakfu na inaambatana na maagano kati ya Mungu na mtu mbele ya watu, na hufanyika madhabahuni sasa huwa hayavunjiki kwani huwezi tena kuwapata wale watu na yale madhabahu ili kuvunja huo wakfu.
Maneno funguo hapa ni ibada,wakfu,agano na madhabahu.(pata maana zake)
Ndiyo maana unaweza kusitisha/kusitishwa kuhudumu,lakini huwezi kutengua.
Mfano uliwahi kuwa mwanajeshi katika ngazi fulani utabaki hivyo kwani ulishajuzwa baadhi ya mambo ambayo hayatakutoka daima.
 
Utafanyaje pact na kiumbe ambacho hakipo?

Huo ni ukichaa kufanya kiapo na kiumbe ambacho haki exist...

Hajawahi ongea na wewe,hajawahi kukutuma chochote,etc...unabaki kuhisihisi tu na kuongea vitu vya kufikirika..."kanituma nije kuwachunga kondoo wake",kakutuma lini?umeongea nae lini?who,why,what and where?Kama sio kuchanganyikiwa tu?
Duuuuuh......wewe hauna dini?
 
Duuuuuh......wewe hauna dini?

Dini?Dada kua serious!

Dini ni group la watu waliojichagua wenyewe kwa utashi wao ili wawatawale wenzao ambao ni waumini!

Sasa basi,DINI ni for stupid people wanaohitaji kutawaliwa na wenzao!

Mungu hayupo,hajawahi ongea na binadamu yeyote kuhusu lolote asilani.Hakuna mwenye ushaidi wowote!Hajawahi tuma mtu au kiumbe chochote kije kifanye chochote hapa duniani,hakuna ushahidi wa hili!

Lets be serious jamani!
 
Hivi mkuu pale panakuwaga na mkeka kweli!? Navyojua mimi ile ni ibada ya kuwekwa wakfu na inaambatana na maagano kati ya Mungu na mtu mbele ya watu, na hufanyika madhabahuni sasa huwa hayavunjiki kwani huwezi tena kuwapata wale watu na yale madhabahu ili kuvunja huo wakfu.
Maneno funguo hapa ni ibada,wakfu,agano na madhabahu.(pata maana zake)
Ndiyo maana unaweza kusitisha/kusitishwa kuhudumu,lakini huwezi kutengua.
Mfano uliwahi kuwa mwanajeshi katika ngazi fulani utabaki hivyo kwani ulishajuzwa baadhi ya mambo ambayo hayatakutoka daima.

Mkeka?Duh!!!!Maajabu ya karne haya!

Maagano na Mungu?Wapi mungu alishakuja kwenye sehemu inayoitwa madhabahu akaweka agano na mtu?Never!

Ni wanadamu waliojichagua wenyewe,walioamua kujikusanya sehemu ya nyumba waliyoiita kanisa,sehem ya mbele yenye ngazi za kupanda walipopaita madhabahu,wakakusanya vijana waliowsomesha madarasani na kuwaambia haya semeni nyie ni mapadre kuanzia leo!

Na hii ya mungu wenu kuchagua kipande kidogo cha ardhi duniani kilichojengwa kitu kinaitwa kanisa ndio mahali pakuweza kuongea nae ni vituko.Huyu Mungu atakua ni binadamu kabisa.

Mungu mchagua a piece of real estate eti ndio nyumba yakena infact hayumo humo,na hajawahi watuma wajenge chochote!
 
Only if you can define the key words then we can be in position to exchange ideas.
 
Only if you can define the key words then we can be in position to exchange ideas.

Key words zipi mkuu!

Tunaongelea holistic nature ya religion.Maana zote zina tabia moja!

Zipo DINI zaidi ya 32,000/= za kikristo.Hizo ni za Kikristo tu,bado milions and millions ya dini zingine.Na zote haziwezi kua za kweli na huyo Mungu!

Mkweli na Muongo ni nani?Kila muumini atasema ni wao,rubbish kabisa!

Niambie wewe unaonaje?
 
Dini?Dada kua serious!

Dini ni group la watu waliojichagua wenyewe kwa utashi wao ili wawatawale wenzao ambao ni waumini!

Sasa basi,DINI ni for stupid people wanaohitaji kutawaliwa na wenzao!

Mungu hayupo,hajawahi ongea na binadamu yeyote kuhusu lolote asilani.Hakuna mwenye ushaidi wowote!Hajawahi tuma mtu au kiumbe chochote kije kifanye chochote hapa duniani,hakuna ushahidi wa hili!

Lets be serious jamani!
Hongera kwa kuwa na imani hiyo
 
Wakati wanapopewa daraja la upadre kulala chini ya mkeka au dhuria maana ake ni kuifia Dunia! Yaani kuikataa dunia na mambo yake yote na kumfata Kristo.kuwa tayari kubeba msalaba nae.
Mapadre wana viapo vya utii,useja(no ndoa) na wengine Ufukara(kuwa watakuwa wasiomikiki mali yeyote ile katika maisha yao wakiwa katika Dunia hii)
Kuwa watii kwa viongozi wao(maaskofu na wakuu wa Mashirika yao(kama wakapuchini,wabenediktini etc)
Nadhani nimeweza kukupa mwanga kidogo
Kiapo cha ufukara siku hizi hakifanyi kazi..
 
Nikiwa kama Kijana Mkatoliki sijawahi kujua kuna siri gani katika viapo vya wahudumu wenu ma Padre.

Je vile viapo vina nini? maana nimeona asilimia kubwa ya mapdre walioacha upadre wakiwa hawapo sawa kiakili yaani kama wamechanganyikiwa flani ivi!

Kingine Kuna ile kama wanalala kwenye mkeka wakati wanaapishwa kuwa Mapadre, ili ku pass upadre inabidi anyanyuke au asinyanyuke!

Kama kuna mtu anajua vyema hapa tafadhali tujuze!
Hao watakuwa walisoma Seminary mpaka level ya philosophy wakaacha kabla ya Theology.. Ndio vichwa vyao huwa havitulizani
 
Upadre ni process ndefu baada ya form six Kuna malezi mwaka mmoja hadi miwili kulingana na jimbo au shirika.Alafu inakuja degree ya Philosophy inayochukua 3years...alafu tena degree ya Theology. Sasa wenye shida ni wale wanao ishia philosophy kwa kuwa philosophy yakufunza ku question kila kitu hata uwepo wa Mungu... Sasa mtu akimaliza Philosophy inabidi apate kitu kama ubatizo kwenye Theology as hapo anamjua tena Mungu...
 
Kuna mzee moja mtaani alikua anavaa smart sana lakini anatembea uku anaongea mwenyewe yani ka zimeruka flani hivi, kuchunguza kumbe alikua padri akaacha lakini anawatoto wapo so successful ila ye ndo hazimo...vile viapo si vya mchezo mchezo
Huenda baada ya kuonja utamu ambao aliukataa kwa miaka mingi ndo alidata na kujutia sana mpaka mpaka akawa punguani.
 
Back
Top Bottom