Ukubali usikubali mpira ni ibada ya sanamu viwanja vinajaa pomoni kuliko nyumba za ibada ya Mungu. Mpira umekuwa ni kiungo muhimu kuunganisha watu mbalimbali kuliko dini zilizozoeleka. Kila kona watu watu wanaongelea mpira. Mpaka wanawake wameingizwa huko tena wanaucheza katika haiba ya kiume kiasi cha kuwa kama wanaume huku wakiachana na haiba ya kike ambayo ni asili yao. Hata kuolewa kwao ni shughuli pevu, watafanyaje mapenzi wakiwa na haiba ya kiume kama si kuwa wapenzi wa jinsia moja? Mpira unatumika kupitisha ajenda mbaya za kishetani na hili lipo wazi linaonekana kuwepo kwa bendera ya kuunga mkono kampeni za mapenzi ya jinsia moja kwenye mchezo wa mpira.
Mkuu! Nadhani inabidi ukae chini uanze kutafakari upya. Punguza kidogo mihemuko.
Hakuna sehemu ambayo shetani hapitishi agenda zake. Nakeambia hivi, haipo na haitakuwepo. Na maandiko yanathibitisha hilo.
Achana na mpira kwanza, twende makanisani kwetu ambako ndiko tunakutana mara kwa mara kumwabudu Mungu. Je, unafikiri huko shetani anakuogopa? Kwamba hafiki? Yupo na anaendelea kupenyeza agenda zake.
Huoni makanisa yanavyoshambuliwa? Huoni mafundisho ya uongo yanavyopyenyezwa makanisani?
Hata kwenye mpira, ambako kuna mkusanyiko wa watu wengi, shetani hawezi kukuacha salama. Maana mtaji wake wa kwanza ni watu.
Yaani kila sehemu yenye mkusanyiko wa watu huo ni mtaji wa shetani kuanzia. Wewe huoni huko ofisini kwako kukoje? Utakuta yanaongelewa masuala ya ngono tu mda mwingi.
Yaani hata wale watu wanakusanyika kufanya kazi ngumu vipi, kama kubeba zege nk, wakishapumzika tu unaona story za ngono na starehe nyingine zinapita. Shetani hawaachi watu wapumue.
So, Ibilisi yupo kila sehemu. Mpira ni sehemu ya mkusanyiko kama ilivyo mikusanyiko mingine. So ibilisi ni dhahili agenda zake zitapitia hapo pia.
Ambacho kinatakiwa ni kwa kila mtu kuwa na uelewa binafsi wa kushinda hoja nyingine za shetani. Mimi ninachokitaka ni mpira wenyewe, yaani zile dakika 90 za kuupiga mpira. Na sio mambo mengine ambayo yako associated na mpira.
Na ninavyoandika hivi, simaaishi namtukuza ibilisi shetani. Hapana. Naonyesha mbinu zake na namna ya kuendelea kumpinga.
Ubarikiwe.