Kuna siri Seif na Mbowe kuhusu kudai Katiba Mpya

Kuna siri Seif na Mbowe kuhusu kudai Katiba Mpya

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,940
Reaction score
7,849
Kwa mawazo yangu ukitaka kuvunja muungano basi uwe na Serikali ya Tanganyika yenye madaraka ya ndani makubwa sawa na ile ya Zanzibar.

Ukifanya hivyo utabakia na serikali ya muungano yenye kudhibiti Wizara chache hazizidi kumi. Serikali ya muungano itakuwa dhaifu tegemezi.

Kama tanganyika nayo ina Rais wake kama zanzibar rais wa muungano sijui atakua na kazi gani. Hapo Rais wa Zanzibar kama hataki Muungano kazi yake ni rahisi tu.

Itakuwa kufanya ukorofi tu karata zinaanguka. Rais wa tanganyika ataweza kuachilia mbali Muungano na kinchi kidogo kinachomsumbua.

Hapo naona ndio ilipo siri ya Maalim Seif na Mbowe au iliyokua CUF ya Seif na CHADEMA kuhusu kudai katiba mpya.

Kwenye Bunge la Katiba walipoona hilo halitatokea wakatimka. Nadhani kuna dili CHADEMA kusaidia kuvunja Muungano kupitia katiba ya Serikali tatu. Bila shaka tumemsikia kichaa Lissu akizungumzia uhuru wa Zanzibar

Watanzania tukae chonjo na vibaraka.
 
Ukitaka kuepuka hilo dawa ni kuipa mamlaka serikali ya muungano ku veto na ku overrule maamuzi ya serikali zote mbili pale inapobidi kwa maslahi ya taifa.

Serikali za majimbo US zina nguvu sana tena zina hadi polisi wake na wanajeshi (sort of) wanaitwa national guard. Lakini federal government inao uwezo wa ku veto maamuzi ya states kwa utaratibu fulani uliowekwa.

Kwahiyo usiwe na hofu, tena serikali tatu ndio njia rahisi zaidi ya kuelekea serikali moja.
 
unafaida kwanini ubunjwe! Lakini kwa mazingira ta Sasa nchi moja unakuwa kma koloni lanmwingine. Acheni uwoga muungano unapaswa kuwa umerichiwa na nchi zote mbili na ni kazi ya viongozi kuwaelimisha wananchi fida za muungano ili watakapotakiwa kupiga kura ya kuridhia ama kuukataa muungano Basi wafanye chaguao Bora kwa mustakabali wait. Mfano si unauona uingereza wananchi ndio wenye nchi na kwa umoja wao waliamua kujitoa kwenye muungano wa umoja wa ulaya (EU).
 
Kwa mawazo yangu ukitaka kuvunja muungana basi uwe na serikali ya tanganyika yenye madaraka ya ndani makubwa sawa na ile ya zanzibar. Ukifanya hivyo utabakia na serikali ya muungano yenye kudhibiti wizara chache hazizidi kumi. Serikali ya muungano itakua dhaifu tegemezi. Kama tanganyika nayo ina rais wake kama zanzibar rais wa muungano sijui atakua na kazi gani. Hapo rais wa zanzibar kama hataki muungano kazi yake ni rahisi tu. Itakua kufanya ukorofi tu karata zinaanguka. Rais wa tanganyika ataweza kuachilia mbali muungano na kinchi kidogo kinachomsumbua.
Hapo naona ndio ilipo siri ya maalim seif na mbowe au iliyokua cuf ya seif na chadema kuhusu kudai katiba mpya. Kwenye bunge la katiba walipoona hilo halitatokea wakatimka. Nadhani kuna dili chadema kusaidia kuvunja muungano kupitia katiba ya serikali tatu. Bila shaka tumemsikia kichaa lisuu akizungumzia uhuru wa zanzibar
watanzania tukae chonjo na vibaraka.
Hongera mkuu, umeongea kama Bashite
 
Siku ukisikia mzanzibari kawa Raisi wa Muungano utaona bara inataka kujitenga.

Nakumbuka hata G45 ilibarikiwa na Bunge la chama kimmoja kupitisha mswaada wa serikali tatu,wakati Ali Hassan Mwinyi akiwa Raisi wa Tanzania.

2025 ni zamu ya Zanzibar, utasikia bara watakuja na katiba ya serikali 3.
 
Back
Top Bottom