Kuna tabia watu kuona wazee ni wachawi. Je, wewe ukizeeka utakubali kuitwa hivyo?

Kuna tabia watu kuona wazee ni wachawi. Je, wewe ukizeeka utakubali kuitwa hivyo?

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Nchi yetu kuna mambo ya ajabu sana pale idadi ya vikwonge kushambuliwa kwa tuhuma za kudai ni wachawi.

hii imejengeka sana tanzania kote na msemo huu ulisha kuwa na mizizi kwa watu ambao bado stage ya kufikia uzee kutumia :" Mzee mchawi, Mzee mwanga"

Je, stage ya uzee ndio stage ya hayo watu wameweka akilini mwao.

Kipindi cha nyuma kulitokea mauaji mengi yanayo shutumu wa wazee kwa sababu ya imani tulizozijijengea.

Kumbukeni imani uliyojijengea na wewe unaenda kuzeeka utakubali au utajisikiaje.
 
... Kanda ya Pwani na Kaskazini ni maeneo ambako wazee wanaheshimika, kupendwa, na kutunzwa sana! Mfano, kwa masai kadiri umri unavyokwenda heshima inakuwa mara dufu. Huko kwingine ndio kuna ujingaujinga fulani hivi kutokana na kuendekeza imani za kipuuzi.
 
Kama ni mchawi ni mchawi tu. Unataka uniambie kila Mzee anaitwa mchawi
 
Iko wazi kama hizi mambo zinaongozwa na VIJANA.. na sio wazee wenyewe .. na hii inaonyesha wazi kuwa vijana wa zama hizi WAMECHANGANYIKIWA yaani hawana akili unakuta mtaani ulipotoka/ulipozaliwa unapoishi kuna vijana mia ila ukijaribu kuchagua wangapi?

Wapo sawa sawa waweza pata 5-7 wengine yaani wanajiendea endea tu mara mibangi/miunga hawaeleweki na ukifatilia ni magraduet karibia wote.. wako ovyo ovyo
 
Mzee mwenzangu Mohamed Said njoo uone hawa Watoto wanataka kutuchoma moto sasa
Kolola,
Nacheka peke yangu kama mwehu.
Mzee mwenzangu mimi naona niko salama kwa ajili ya ''life style,'' yangu.

Sidhani kama hawa vijana wa hapa mtaani kwangu Magomeni Mapipa wanaweza kunidhania mimi kuwa ''Gagula.''

Sijui wewe mwenzangu uko wapi.
Kijiini?
 
Mtu kazaliwa kwenye eneo fulani, kasoma hapo, kapata ki boda boda anaendesha hapo hapo, anampa mimba binti hapo hapo, wanaenda kuishi kinyumba eneo la hapo hapo, mambo hayanyooki anaanza kulaumu wazee wa mtaa wa hapo hapo wanamroga,

Kijana ukishamaliza shule hama eneo lenu kajichanganye sehemu zingine, rizki zipo kila pembe ya dunia, jifunze kutembea utajifunza mengi na sio kujifungia kwenye debe.
 
Hao ni watu wanaokwepa majukumu ya kuhudumia wazee wao.
Nimeiona Sana, unakuta Baba au mama mdogo, shangazi au mjomba ambaye hakuoa au hakupata watoto,

Umri umekwenda anahitaji msaada wa watoto wapwa, huyo atapata taabu Sana ya kunyanyapaliwa na kuitwa mchawi ilimradi watu wamtenge, ni tabia mbaya sana.

Kibaya zaidi, unakuta huyu anayeitwa mchawi ndiye aliyewalea na kuwahudumia, sasa asiwanyonge wakati wapo wadogo aje awachawie!
Ifike mahali ramli chonganishi iwe jinai!
 
Kolola,
Nacheka peke yangu kama mwehu.
Mzee mwenzangu mimi naona niko salama kwa ajili ya ''life style,'' yangu.

Sidhani kama hawa vijana wa hapa mtaani kwangu Magomeni Mapipa wanaweza kunidhania mimi kuwa ''Gagula.''

Sijui wewe mwenzangu uko wapi.
Kijiini?
Wazee mkae chonjo, vijana wamevurugwa na uchumi wa kati
 
Kolola,
Nacheka peke yangu kama mwehu.
Mzee mwenzangu mimi naona niko salama kwa ajili ya ''life style,'' yangu.

Sidhani kama hawa vijana wa hapa mtaani kwangu Magomeni Mapipa wanaweza kunidhania mimi kuwa ''Gagula.''

Sijui wewe mwenzangu uko wapi.
Kijiini?
Mimi nipo kijijini huku Nakutogagwa na kwa vile bi mkubwa alinikimbia huwa napika mwenyewe. Taabu ni kuwa usukumani hatuna kuni na njia ya kupika ni kutumia samadi ya ng'ombe.

Macho yangu mekundu na tumbo limejisokota nina negative kitambi. Mavazi yenyewe Allah ndiye anjua. Sijui kama nitapona kuitwa mchawi
 
Nkoyi!
 
Back
Top Bottom