Kuna tatizo gani TRA kwenye EXIGA

Dumelang

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
3,204
Reaction score
5,710
Subaru Exiga, Hizi ni gari zilizotolewa kuanzia mwaka 2008.

Ni gari nzuri kwa familia kwakweli, Tangu mwaka juzi nimekuwa nikiangalia Kodi yake kwenye calculator ya TRA, kodi haipungui mil 20 huku wakikadria ina CIF ya USD 8000

Ukweli wa gari hii zimejaa kwenye web za mauzo ya magari ya japan, nyingi na hazina hata CIF ya USD 3000, nyingi hata za 2010, FOB yake ni mpk usd 600 kuendelea mpk usd 1800 FOB

Sasa swali langu kwenu wadau na TRA particulary kuna tatizo gani mpaka iwe na makadrio ya juu hivi?

Mwaka 2016 niliwatumia email huduma kwa mlipa kodi kuomba wafanye review ya hio gari lakini bahati mbaya haikujibiwa.

Kama kuna wenye ufahamu humu ama maafisa wa TRA tusaidieni. Tujue

#picha zote kwa hisani ya SBT Japan
 
Hatimae TRA wasikia Ombi Langu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kwa juhudi zako kuzaa matunda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…