Kuna 'teja' kwa kila familia Zanzibar-BBC utafiti.

Kuna 'teja' kwa kila familia Zanzibar-BBC utafiti.

GT kama kweli upo Unguja hii tathimini ya BBC unaikataa unaonekana wewe ni mbishi wa asili au la upo mbali na jamii ya WASHIRAZI. But for me naikubali kwa 90% kuwa ni ukweli shukuru Mungu familia yako haijaadhirika na hilo janga but Most of young man huko unguja wanatumia sana madawa ya kulevya hii yote wanaifanya kutafuta mbadala wa pombe.Unguja niijuavyo mimi kijana avutae bangi/*******/****** anaonekana msafi kimaadili kuliko anaye kunywa pombe.


unajua maana ya ``washirazi``

washirazi maana yake ni watumwa waliopewa nguvu na wana mapinduzi

unajua maana ya ``mapinduzi``
mapinduzi ni yale yalioletwa kutoka bara na waliofanya mapinduzi ni wabara na kuwapa washirazi waharibifu wa zanzibar.

chama cha mapinduzi asili yake bara (mapinduzi daima) ndio ukaona kila uchaguzi jeshi kutoka bara pamoja na polisi

bbc pale karume aliposema suala la muungano waulizwe wazanzibar wa kweli walishindwa kumuuliza

1. yupi mzanzibar wa kweli?
2.asili yake yeye ni wa kweli au wa uongo?
3.vipi pale wazanzibar walipomkataa?
4.au wazanzibar ni watanganyika wale waliomueka?

lakini bbc pale walipoligusia suala la muungano walifukuzwa zanzibar na smz
na wale waliowapata kuupenda muungano ni wahamiaji watupu wanaokaa bila ya sheria na kufurahia zanzibar

unga unaonjeshwa kwanza bure pale unapokuwa na mashaka ya kimaisha na dili hii imetokana na washirazi na wanamapinduzi ili kuwamaliza wazanzibar.

na vyombo vya usalam wote wanajua suala hilo na kila duka wanalijua lakini ni ajenda isiyo ya siri inajulikana
 
Baa tena? Fanya utembelee huko! Zenj hakuna taputapu, ndio maana tende ipo juu baada konyagi...
Zamani zile Mahonda iliokoa wengi na Sundown zao....


umechelewa patupatu imeingia toka 1964 imeletwa na wamakonde

alafu nikuulize? wewe mmakonde nini?

kuna pombe mpaka inayotengezeza mkojo
 
..inawezekani ni interpretation tu ya data za idadi ya mateja wa unga vs idadi ya kaya ZNZ.

..inawezekana kuna familia hazina mateja kabisa, halafu nyingine zina mateja 2 au 3, nyingine teja mmoja etc etc.

..unapoambiwa kwamba asilimia 25% ya mji fulani wana virusi vya ukimwi, haina maana kwamba lazima, lazima, kila penye mkusanyiko wa watu 100 ktk mji huo, 25 watakuwa na vvu. idadi hiyo inaweza kupanda au hata kupungua ktk mkusanyiko huo.


..tatizo hili inaonekana lipo ZNZ. sasa ni vyema likashughulikiwa hata kama si kubwa kama lilivyoripotiwa BBC.


kuna familia nyiengine zote teja.

kuanzia baba, mama na watoto.

na ukikosa hapo bazi wengine wizi familia nzima
 
BBC ni idhaa ya propaganda za ukiristo na ukafiri kwa ujumla ikiwa nyuma ya pazia la umagharibi. Hakuna mateja kwa kila familia Zanzibar, kauli hii ni ya Kijahili.
 
BBC ni idhaa ya propaganda za ukiristo na ukafiri kwa ujumla ikiwa nyuma ya pazia la umagharibi. Hakuna mateja kwa kila familia Zanzibar, kauli hii ni ya Kijahili.
Weeeeeeeee usilete habari za udini kwenye hii la mateja na unguja.
mzee hili swala haliusiani na udini hata kidogo na ni ukweli mtupu kaka.
Mimi ni ustaadhi wa swala tano, ungeelekeza lawama kwa serikali ya SMZ na wala siyo propaganda. wewe wa wapi?
 
sisi familia yetu iko unguja na hakuna mbwia unga

typical BBC

washakosa cha kuripoti

hivi na wao tukisema kuwa BBC swahili kumejaa walevi na wazinzi watakubali?

GT ni mmoja ya wachangiaji ninaowakubali sana, lakini kwa hili, I have to dis-credit you mkuu!!!!!!!!!!!

Wanaposema kila familia, that is on average basis! Inawezekana hata familia kumi hazina hata mbwia unga lakini ukakuta familia nyingine kumi kuna kila familia mateja 3! ndio maana wakasema kila familia ina teja.

Usinifanye niamini kwamba hukuwahi kufanya research huko ulikopita!!
 
Back
Top Bottom