Tetesi: Kuna Tetesi za kufanyika mabadiliko ya Utawala Zanzibar

Tetesi: Kuna Tetesi za kufanyika mabadiliko ya Utawala Zanzibar

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,291
Kuna tetesi zinaendelea kuzagaa kule Zanzibar kuhusu kufanyika mabadiliko ya Utawala . Taarifa zinasema kunatarajiwa kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa hivi karibuni zitakazowashirikisha CCM na CUF.

Vyanzo vyetu vinadokeza kumekuwa na usiri mkubwa wa jambo hili baina ya pande mbili na usiri wa walio nyuma ya mpango huo zikihusishwa jumuiya za kimataifa kwa kushirikiana na mamlaka za ndani.

Siku za hivi karibuni kwa upande wa CUF, viongozi wa Zanzibar wamezidisha juhudi za kuwaeleza wanachama wao kile wanachokiita haki yao na kutumia kurugenzi zao za uchaguzi na usalama na ulinzi kuzunguka wilaya zote za Zanzibar kuwatayarisha kupokea mabadiliko. Kuna vikao vingi vya ndani vimefanyika na hadi kufikia kuwaarifu kujiandaa kupamba.

Na kwa upande wa CCM kuna taarifa za kuwa na vikao vingi ingawa usiri umezidi juu ya kile hasa kinaendelea.

Tetesi hizi zilizidi baada ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif kuarifu kwamba alitarajia isingezidi miezi mitatatu kutoka Agosti 2017 kwamba haki ya wazanzibari ingepatikana ingawa iliarifiwa baadae kwamba siku zilisogea na kusogezwa mbele.

Kinachoendelea sasa ni ukimya na minongono mingi katika vounga vya Zanzibar bila ya kuonekana dalili yoyote ya matayarisho ya mabadiliko.


Wenye taarifa tunaomba ufafanuzi.


Kishada.
 
Seif amekubali kupima mkojo? Mpaka apimwe ndo ataruhusiwa kuingia ikulu.
 
Aisee Seif naye kazidi kuwadanganya wazenji
aache uongo .anawakwamisha wazenji
 
Kwa dongo la mkulu siku ya kuzima mwenge zenji, alisema kuna watu wanasubiri eti kuapishwa sijui wataapishwa lini.!? sahau hio kitu mkuu.!
 
Zilianza tetesi za dr shein kujizuru na kumuachia nchi Seif, naona sasa hivi zimekuja za serikali ya mseto.
 
Wikiendi iliyopita Naibu katibu Mkuu wa CUf Zanzibar alinukuliwa akiwachallenge viongozi wa CCM waje hadharani kama afanyavyo Maalim Seif wakane kama hakuna kitu cha namna hiyo.

Wenye taarifa rasmi twambieni.
 
Back
Top Bottom