Tetesi: Kuna Tetesi za kufanyika mabadiliko ya Utawala Zanzibar

Tetesi: Kuna Tetesi za kufanyika mabadiliko ya Utawala Zanzibar

Sijui kama ni kweli, lakini nafikiri huo mpango haupo.

Jitahidi ufuatilie ili utuarifu ikiwa unaweza kupata habari za ndani za wahusika. Wengine wanaleta hasira kwa mtoa mada ambaye ameleta hizi tetesi tu ili kuhabarisha wana JF.
 
Mkuu acha hizo. Sijaarifu kuwa Zanzibar hakuko shwari au si salama hapana. Kuna tetesi tu za mabadiliko ya utawala. Hiki ndicho nilichosema.

Oya unataka nisemeje unielewe? Mbona unakuwa na Kichwa ' tofali ' hivyo na mgumu kuelewa? Hata kama hakuna hali mbaya ya Kiusalama huko ila hata hayo mabadiliko unayoyasema na kuyashikia bango katika ' Utawala ' wa Zanzibar haupo. Umedanganywa tena vibaya sana. Pole!
 
Wewe jamaa inaelekea mrahisi kudanganyika!kwa style ya CCM hii hauhitaji kuwa mnajimu kujua hilo haliwez kutokea
 
Chini ya JPM hakuna fyokofyoko. Wasubiri 2020 goli lingine.

Kinachotia wasiwasi ni kuwa kuna Viongozi wa upinzani wanapita wilaya zote na kuarifu wala hawaitwa wala kuhojiwa jambo ambalo tunaamini itakuwa ndizo fyokofyoko hizo. Tunasikia hata baadhi ya wana CCm wanawalaumu viongozi wao kwa nini hawa waachiwe bila kuulizwa? Fuatilia siasa za zanzibar.
 
Oya unataka nisemeje unielewe? Mbona unakuwa na Kichwa ' tofali ' hivyo na mgumu kuelewa? Hata kama hakuna hali mbaya ya Kiusalama huko ila hata hayo mabadiliko unayoyasema na kuyashikia bango katika ' Utawala ' wa Zanzibar haupo. Umedanganywa tena vibaya sana. Pole!
Sijashika bango. Hii tetesi isikutoe udenda. Chukulia ni tetesi tu.
 
Wewe jamaa inaelekea mrahisi kudanganyika!kwa style ya CCM hii hauhitaji kuwa mnajimu kujua hilo haliwez kutokea

Mimi sidanganyiki ndio maana nataka nipate ukweli. Kama una taarifa rasmi weka hapa JF.
 
Sijashika bango. Hii tetesi isikutoe udenda. Chukulia ni tetesi tu.

Sasa kama kumbe hata Wewe unajua ni Tetesi kwani unashupalia hadi mishipa ya Ulimini Kwako imekusimama? Naona unanichosha tu.
 
Zbar kwa Wa Zbar...waelewane nchi isonge mbele......!!! Tuwatakieheri......amaniitawale ndani nchi yao......wenye haki wapewe haki pia !!! Wafanye mseto milele....kila uchaguzi waangalie nani ana nyingi....aongoze nchi mwingine Makamu!!! Tuwaaachie

wengine wanafurahia kilichotokea Zanzibar. Hawana habari ya umoja, haki na uzalendo wa kweli.
 
Huyu mtoa mada anaweza kuwa seif.manake seif anajua sana kupiga fix watu wake
 
Kwani si tuliambiwa Seif angejiapisha? Kwa nini serikali ya umoja? Ina maana hajiapishi tena?
 
Mimi sidanganyiki ndio maana nataka nipate ukweli. Kama una taarifa rasmi weka hapa JF.
Tafuta hotuba ya Rais akiwa Zanzibar siku ya kuzima Mwenge kuhusu kuapishwa Seif
 
Ya Zanzibar tuachieni wenyewe Lkn mwisho Wa maji tope
 
Mijiaskari toka bara ndio inakuja huku kwetu kuumiza watu wakati sisi wenyewe tunapendana...sauti ilisikika ndani ya boat
 
Kwani si tuliambiwa Seif angejiapisha? Kwa nini serikali ya umoja? Ina maana hajiapishi tena?

Katiba ya Zanzibar intambuwa Serikali ya umoja wa Kitaifa (SUK), Hata ingekuwa hivyo hilo ni sharti la KATIBA
 
Tafuta hotuba ya Rais akiwa Zanzibar siku ya kuzima Mwenge kuhusu kuapishwa Seif

Niliambiwa kuwa haikuwafurahisha wale wahafidhina kule Zanzibar, eti walitarajia siku hio anange zaidi ya ile ya fyokofyoko, Kuna watu walitaka siku hiyo litoke duku duku la Kumnanga Maalim Seif na kukanushwa yote yale aliyoyasema ambayo bado hayajajibiwa.
 
Back
Top Bottom