Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wavunje vyama vyao vya asili ili watengeneze chama kipya chenye muunganiko wa CCM/CUF.Zbar kwa Wa Zbar...waelewane nchi isonge mbele......!!! Tuwatakieheri......amaniitawale ndani nchi yao......wenye haki wapewe haki pia !!! Wafanye mseto milele....kila uchaguzi waangalie nani ana nyingi....aongoze nchi mwingine Makamu!!! Tuwaaachie
Mkuu usibishane na huyoo...waga anajifanya mtabiri ,alitabiri kitu kibaya sana juu ya MTU fulani lkn haikutokea,akaukimbia uzi wake.Sijashika bango. Hii tetesi isikutoe udenda. Chukulia ni tetesi tu.
Hizo ndoto zako una ota mchana Lazima washughulikie Tatizo la Bara kwanzaKuna tetesi zinaendelea kuzagaa kule Zanzibar kuhusu kufanyika mabadiliko ya Utawala . Taarifa zinasema kunatarajiwa kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa hivi karibuni zitakazowashirikisha CCM na CUF.
Vyanzo vyetu vinadokeza kumekuwa na usiri mkubwa wa jambo hili baina ya pande mbili na usiri wa walio nyuma ya mpango huo zikihusishwa jumuiya za kimataifa kwa kushirikiana na mamlaka za ndani.
Siku za hivi karibuni kwa upande wa CUF, viongozi wa Zanzibar wamezidisha juhudi za kuwaeleza wanachama wao kile wanachokiita haki yao na kutumia kurugenzi zao za uchaguzi na usalama na ulinzi kuzunguka wilaya zote za Zanzibar kuwatayarisha kupokea mabadiliko. Kuna vikao vingi vya ndani vimefanyika na hadi kufikia kuwaarifu kujiandaa kupamba.
Na kwa upande wa CCM kuna taarifa za kuwa na vikao vingi ingawa usiri umezidi juu ya kile hasa kinaendelea.
Tetesi hizi zilizidi baada ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif kuarifu kwamba alitarajia isingezidi miezi mitatatu kutoka Agosti 2017 kwamba haki ya wazanzibari ingepatikana ingawa iliarifiwa baadae kwamba siku zilisogea na kusogezwa mbele.
Kinachoendelea sasa ni ukimya na minongono mingi katika vounga vya Zanzibar bila ya kuonekana dalili yoyote ya matayarisho ya mabadiliko.
Wenye taarifa tunaomba ufafanuzi.
Kishada.
Hivi hawa jamaa watakuwa na uchaguzi 2020 au 2021??Mmmhh, sidhani aisee.
Hapa tusubiri tu 2020
Hahahaa ulishaleta habari nne hapa ya kuwa mtakabidhiwa serikalini karibuni..na zote nilikuambia uwache kuwadanganya watu.. la leo naona umekuja na habari tofauti kidogo na zilizopita kwa kusema serikali ya umoja wa kitaifa.Inawezekana una nia nzuri kwa wafuasi wako ya kuwa hutaki uwape habari moja kwa moja ya kuwa musubiri uchaguzi au mnavuta muda kwani mmeshawadanganya sana kwa kwa upumbavu wao wamewaamini sana then kuwapa habari ya hafla tu ya kuwa sefu amepwerewa na hakuna kitu kwani uwongo wake umefikia tamati unaweza kuwauwa watu.. then kuwazoesha kwa kuwaambia kutakuwa na serikali ya umoja wa kitaifa na baada wala realize wenyewe jinsi walivyokuwa wapumbavuKuna tetesi zinaendelea kuzagaa kule Zanzibar kuhusu kufanyika mabadiliko ya Utawala . Taarifa zinasema kunatarajiwa kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa hivi karibuni zitakazowashirikisha CCM na CUF.
Vyanzo vyetu vinadokeza kumekuwa na usiri mkubwa wa jambo hili baina ya pande mbili na usiri wa walio nyuma ya mpango huo zikihusishwa jumuiya za kimataifa kwa kushirikiana na mamlaka za ndani.
Siku za hivi karibuni kwa upande wa CUF, viongozi wa Zanzibar wamezidisha juhudi za kuwaeleza wanachama wao kile wanachokiita haki yao na kutumia kurugenzi zao za uchaguzi na usalama na ulinzi kuzunguka wilaya zote za Zanzibar kuwatayarisha kupokea mabadiliko. Kuna vikao vingi vya ndani vimefanyika na hadi kufikia kuwaarifu kujiandaa kupamba.
Na kwa upande wa CCM kuna taarifa za kuwa na vikao vingi ingawa usiri umezidi juu ya kile hasa kinaendelea.
Tetesi hizi zilizidi baada ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif kuarifu kwamba alitarajia isingezidi miezi mitatatu kutoka Agosti 2017 kwamba haki ya wazanzibari ingepatikana ingawa iliarifiwa baadae kwamba siku zilisogea na kusogezwa mbele.
Kinachoendelea sasa ni ukimya na minongono mingi katika vounga vya Zanzibar bila ya kuonekana dalili yoyote ya matayarisho ya mabadiliko.
Wenye taarifa tunaomba ufafanuzi.
Kishada.
Catalonia baby!Zanzibar nako wanataka nusu Mkate?
Kutokuja hadharani kupinga anayoyasema Seif haimaanishi kuwa ni kweli anachosema Seif. Kumbuka, Wanae tangu 95 wakimchezea ndevu, anaejihangaisha ni yeye Maalim kukaa hadharani akiwaahidi watu. CCM hawana haja ya kumjibu mana ata wakimjibu watapata nini?Wikiendi iliyopita Naibu katibu Mkuu wa CUf Zanzibar alinukuliwa akiwachallenge viongozi wa CCM waje hadharani kama afanyavyo Maalim Seif wakane kama hakuna kitu cha namna hiyo.
Wenye taarifa rasmi twambieni.