Tetesi: Kuna Tetesi za kufanyika mabadiliko ya Utawala Zanzibar

Tetesi: Kuna Tetesi za kufanyika mabadiliko ya Utawala Zanzibar

Nina sikitika CUF imekuwa kama toothles Dog..
 
Kuna tetesi zinaendelea kuzagaa kule Zanzibar kuhusu kufanyika mabadiliko ya Utawala . Taarifa zinasema kunatarajiwa kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa hivi karibuni zitakazowashirikisha CCM na CUF.
Hayo maradhi ya akili mnayoumwa ni mabaya sana,sefu amewaharibu akili zenu kufikia hatua ya kuishi kama mazezeta
 
Mkuu kama sio ndoto basi ni shibe ya dona na kibua huwa ina maluweluwe kweli.
 
Mkuu kama sio ndoto basi ni shibe ya dona na kibua huwa ina maluweluwe kweli.
Mkuu hakuna haja ya kubeza.

Tetesi za aina hii sio ngeni. Mazingira ya Zanzibar ya miaka ile ya 2009 na kuja mabadiliko ya Katiba yanafafana na haya. Uadui uliokuwepo Zanzibar ni mkubwa sana lakini mwishowe KATIBA ILIREKEBISHWA na kufanywa suluhu ya kudumu.

Siwezi kupuuza tetesi hizi kirahisi.
 
Kuna tetesi zinaendelea kuzagaa kule Zanzibar kuhusu kufanyika mabadiliko ya Utawala . Taarifa zinasema kunatarajiwa kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa hivi karibuni zitakazowashirikisha CCM na CUF.

Vyanzo vyetu vinadokeza kumekuwa na usiri mkubwa wa jambo hili baina ya pande mbili na usiri wa walio nyuma ya mpango huo zikihusishwa jumuiya za kimataifa kwa kushirikiana na mamlaka za ndani.

Siku za hivi karibuni kwa upande wa CUF, viongozi wa Zanzibar wamezidisha juhudi za kuwaeleza wanachama wao kile wanachokiita haki yao na kutumia kurugenzi zao za uchaguzi na usalama na ulinzi kuzunguka wilaya zote za Zanzibar kuwatayarisha kupokea mabadiliko. Kuna vikao vingi vya ndani vimefanyika na hadi kufikia kuwaarifu kujiandaa kupamba.

Na kwa upande wa CCM kuna taarifa za kuwa na vikao vingi ingawa usiri umezidi juu ya kile hasa kinaendelea.

Tetesi hizi zilizidi baada ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif kuarifu kwamba alitarajia isingezidi miezi mitatatu kutoka Agosti 2017 kwamba haki ya wazanzibari ingepatikana ingawa iliarifiwa baadae kwamba siku zilisogea na kusogezwa mbele.

Kinachoendelea sasa ni ukimya na minongono mingi katika vounga vya Zanzibar bila ya kuonekana dalili yoyote ya matayarisho ya mabadiliko.

Wenye taarifa tunaomba ufafanuzi.

Kishada.

Sasa CUF yenyewe si imegawanyika?
Ni muungano wa CCM na CUF ya Lipumba au CUF ya Seif Sharif?!
 
Kwa wanaofutailia siasa za Zanzibar bado kuna masuali mengi.

Kwa mtazamo wangu ishu ya Zanzibar in maslahi ya jumuiya ya kimataifa. Hawa jamaa waliinvest kule hadi maridhiano yakawekwa KIKATIBA. Kwamba Serikali itaongozwa kwa Ushikiano SUK. Haingiii akilini juhudi hizi baada ya miaka mitano tu ya utekelezaji zivunjwe na JECHA kwa maslahi ya CCM na kusiwe na juhudi zile zile .

Naamini wapo walezi wa hili na kiburi imekuwa hulka za viongozi wa kiafrika. Bado naamini uchaguzi wa 2015 Zanzibar na kile kilichotokea kimeacha masuali kwa wanademokrasia wa Dunia na nini imani LAZIMA KUNA KITU NYUMA YA PAZIA.

Siwezi kupuuza pia ahadi za mkongwe wa siasa (Maalim Seif) na mtaalamu hasa wa siasa za ukanda huu kuwa eti anabwabwaja bure na kujivunjia heshima kwa ahadi zile. Siwezi kabisa.

Tetesi zinazoendelea lazima zitaaacha zitawaumbuwa hawa wadau ama CUF au CCM kule Zanzibar.

Logics hazikubali tatizo la Zanzibar kuachwa bure bila kutafutiwa ufumbuzi na hao walioinvest hadi kuja GNU.

Hapa ndipo hizi tetesi zinapopata nguvu.

wengine wanatoa povu bure.
 
As long as KATIBA YA ZANZIBAR imevunjwa. sasa hivi hakuna GNU wala hakuna V- I na wala mawaziri hawatokani na akidi ya chama kilichoongoza kwa ratio ya chama kiklichofuata kama yalivyo masharti ya KATIBA YAO.

Kuna gap katika muundo wa SMZ ya GNU. Hili moja.

Lengine kuna kawaida moja ya hawa wazungu kuishi ndani ya Principles zao. Hili la Zanzibar lilishatoewa msimamo kwa Tanzania kunyimwa misaada ya maendeleo. Ahadi hizi zinazotolewa leo sio bure. Lazima wangetoa ufafanuzi ama kuenguwa maamuzi yao. Vyenginevyo eneo hili la ahadi za wazungu kwa Tz zinatoa Clue nyengine kuwa inawezekana kuna kitu kwenye process.

Bado siwezi kupuuza tetesi hizi kirahisi katika misingi ya maelezo yangu haya.
 
Sasa CUF yenyewe si imegawanyika?
Ni muungano wa CCM na CUF ya Lipumba au CUF ya Seif Sharif?!

Unaweza usiamini waliouunda mgogoro huo wanajuwa watauondowa vipi pale watakapoona inafaa. Hizo ni kazi za system tu.
 
Hayo maradhi ya akili mnayoumwa ni mabaya sana,sefu amewaharibu akili zenu kufikia hatua ya kuishi kama mazezeta

Waulize wana CCM wa Zanzibar namna walivyo na hofu na kauli za tetesi hizi.
 
Kuna tetesi zinaendelea kuzagaa kule Zanzibar kuhusu kufanyika mabadiliko ya Utawala . Taarifa zinasema kunatarajiwa kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa hivi karibuni zitakazowashirikisha CCM na CUF.

Vyanzo vyetu vinadokeza kumekuwa na usiri mkubwa wa jambo hili baina ya pande mbili na usiri wa walio nyuma ya mpango huo zikihusishwa jumuiya za kimataifa kwa kushirikiana na mamlaka za ndani.

Siku za hivi karibuni kwa upande wa CUF, viongozi wa Zanzibar wamezidisha juhudi za kuwaeleza wanachama wao kile wanachokiita haki yao na kutumia kurugenzi zao za uchaguzi na usalama na ulinzi kuzunguka wilaya zote za Zanzibar kuwatayarisha kupokea mabadiliko. Kuna vikao vingi vya ndani vimefanyika na hadi kufikia kuwaarifu kujiandaa kupamba.

Na kwa upande wa CCM kuna taarifa za kuwa na vikao vingi ingawa usiri umezidi juu ya kile hasa kinaendelea.

Tetesi hizi zilizidi baada ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif kuarifu kwamba alitarajia isingezidi miezi mitatatu kutoka Agosti 2017 kwamba haki ya wazanzibari ingepatikana ingawa iliarifiwa baadae kwamba siku zilisogea na kusogezwa mbele.

Kinachoendelea sasa ni ukimya na minongono mingi katika vounga vya Zanzibar bila ya kuonekana dalili yoyote ya matayarisho ya mabadiliko.

Wenye taarifa tunaomba ufafanuzi.

Kishada.
Maalim Seif atulie ajipange 2020 labda ndoto zake zitatimia kabla hajaondoka duniani.
 
Naona wengi wana kana kama kuna mienendo mizitio na mabadiliko yanakuja. Kipi kisicho wezekana. Wameiba KURA mchana. CCM zanzibar wameshindwa vibaya sana, na shida ni kuwa walikabidhi vyeti kwa washindi. Sasa wale waliokabidhiwa vyeti ndio wawakilishi halali wa wananchi. Kwa hivo, taarifa zote zipo wazi na CCM wameshindwa kujitetea katika wizi huu. Hilo la kwanza. La pili ni kuwa kesi ya muungano katika korti ya afrika mashariki, serikali wameshindwa kujieleza kwa nini muungano usivunjike. Kwa hiyo, munaweza kuchewelesha mabadiliko lakini mabadiliko ni lazima na yapo.
 
Wavunje vyama vyao vya asili ili watengeneze chama kipya chenye muunganiko wa CCM/CUF.
Kwanza wapatane na kuweka pembeni wa bara maana kuna unafiki sana kwa wanaofaidika na mfumo toka Bara.....wakijielewa hapo ndio wataweza kwenda kwenye Taifa lao huru
 
seif amezidi upole siku izi
tapatalk_1509282710994.jpeg
 
Kwa dongo la mkulu siku ya kuzima mwenge zenji, alisema kuna watu wanasubiri eti kuapishwa sijui wataapishwa lini.!? sahau hio kitu mkuu.!
Sio wa kumwamini sana.... hakawii kukana kauli zake.!
 
Nimesikia CCM wakisema Seif anatakiwa akapime akili....
 
Back
Top Bottom