Kuna tofauti gani kati ya 4WD na AWD?

Ningependa maelezo kwa lugha ya kiswahili mkuu.
Maelezo ya kizungu nimeenda Google nimeyakuta.
Tofauti kati ya AWD na 4WD ni kwamba AWD huwashwa kila wakati huku unaweza kubadilisha kati ya kuwasha na kuzima 4WD. 4WD ni nyongeza ambayo kwa kawaida utapata kwenye lori, huku AWD ikitumika zaidi kwa magari na SUV
 
AWD -All wheel drive. Manake maringi yote yanasukuma gari. Kuna full time AWD na part time AWD. Full time km jina, muda wote Huwa maringi manne yanafanya kazi ya kusukuma gari na part time huwa aidha ya mbele yatasukuma gari pekee au ya nyuma ndio yatafanya hio kazi kutegemea na vile sensors zitakavoona Bora. Kwaio wewe km dereva wewe endesha tu, gari itaamua wenyewe kupeleka power ringi za mbele au nyuma ikiwa part time AWD na ikiwa full time ndo utulie tu gari ishaamua kupeleka power Kwa maringi yote.

4wd - 4 wheel drive. Nayo pia maringi yote yanauwezo wa kusukuma gari. Ila hii inakupa more control, kama hutaki yote yasukume gari, una chagua utakavyo. Kama unataka system ya off-road basi 4wd ni bora. Ila performance wise kama unataka sedan AWD ni nzuri.

In short chukulia AWD ni automatic 4 wheel drive [emoji28]
 

Asante mkuu.
Nimepata mwanga.
 
Mkuu, umeelezea vizuri lakini umechanganya kidogo.

Iko hivi 4WD ni mfumo ambaoo tairi zote nne za gari zinapokea nguvu kutoka katika engine kupitia gear box. Mfumo huu wa uendeshaji wa matairi upo katika aina mbili:-

Part time 4WD, hii inakua inatumika pale ambapo dereva anaona kuna uhitaji wa kutumia tairi zote kuendesha gari hasa katika mazingira korofi kama tope au mchanga, hii inawezeshwa na kitu maalumu kinachoitwa limited slip differential,dereva atabadili kutoka 2WD kwenda 4WD kwa kutumia stick kutoka maalum iliyo pembeni kidogo mwa gear shift stick.

Full time 4WD, hii matairi yote manne yanaendesha gari na dereva hana option ya kuchagua kurudisha kutumia 2WD na hii ndio ilianza baadae ikaja kua modified na kupatikana part time 4WD.


AWD, (All wheel drive), huku sasa gari inaendesha kwa kutumia tairi zote nne na dereva hana uhuru wa kubadilisha kutumia tairi mbili, utofauti wa hii na 4WD ni kua mfumo huu una sensors ambazo kwa wakati wake zinaipa gearbox taarifa ni wapi pa kupeleka nguvu zaidi. Kwa mfano tairi ya kulia nyuma ya gari ikinasa basi sensors itaiambia gari ipeleke nguvu nyingi huko na kutopeleka kabisa au kidogo kwa tari zingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…