Kuna tofauti gani kati ya Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali ya Rufaa?

Kuna tofauti gani kati ya Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali ya Rufaa?

Kijiji kinahudumiwa na zahanati, ikishindikana hapo hupelekwa kituo cha afya ambacho huudimia vijijiji kadhaa hapa huduma huongezeka madaktari wa degree huanzia kwenye ngazi hii.

Tatizo lisipotatuliwa hapa mtu hupata rufaa kwenda hospitali za wilaya, kisha mkoa na mwisho hospitali za rufaa. Tiba isipopatikana hapa kwa hapa nchni hupelekwa hospitali za juu kabsa hususani muhimbili.

Ngazi hizi hutofautiana kwa watu wanaoziendesha, madawa na vifaa. Kuna vifaa na dawa huvipati zahanati ila ukienda kituo cha afya utazikuta. Vile vile zipo huduma mikoani na rufaa huzikuti kituo cha afya.
 
Zahanati,kituo cha afya hospital ya wilaya ,hospital ya wilaya,hospital za mkoa na hospital za rufaa
 
Kwahiyo zahanati ni kitu kimoja na kituo cha afya ama! Na kama ni tofaut tofaut ni nini?
Kijiji zahanati

kata kituo cha afya ngazi hii kuna uwepo wa MD AMO Co huduma ya upasuaji kwa akina mama dental clinic nk
 
Kwa set up ya Huduma za Afya za Umma Lengo Ni:-
Kila Kijiji kiwe na Zahanati
Kila Kata iwe na Kituo Cha Afya
Kila Wilaya iwe na Hospitali ya Wilaya (Ya serikali,au kama haipo Serikali itaingia Mkataba na Hospitali ya Shirika la dini)
Kila Mkoa uwe na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (Regional Referral Hospital-RRH)
Kila Kanda Kutakuwa na Hospitali ya Rufaa (Mfano KCMC ,Bugando,Mbeya Referral etc
Kwa Taifa tuna National Hospital
Pia kuna Specialised Hospitals (Mfano Jakaya Kikwete Heart Institute, Mkapa Hospital, Etc)

Anatakiwa mgonjwa aanzie zahanati,kisha apande juu kama hakupata nafuu (Ingawa kwa Dar watu huanzia hata Muhimbili au Hospitali za Wilaya (Temeke,Amana,Mwananyamala) ambazo kuanzia Julai 1 Nazi zitakuwa Categorized Kama RRH,na hivyo kuondoka Tamisemi na kuwa Chini ya wizara ya Afya.

Aina ya Wataalam,Vifaa na Huduma zinatifautisha level moja na nyigine.
 
Hospitali ya rufaa huwa na madaktari bingwa na vifaa bora. Tatizo kilikoshindikana huko kote linakuwa referrered kwenye hospitali kubwa
mimi nafanya kazi mochwari tungekuwa ofisi moja ninge kutolea balimi kwenye jokofi la maiti upoze kiu kwa kwa mfafanulia
 
Kwahiyo zahanati ni kitu kimoja na kituo cha afya ama! Na kama ni tofaut tofaut ni nini?
Zahanati

kunakua na medical oficers wenye diploma, wanaitwa clinical oficers, na walikuepo pia wenye certificate rural medical officer kama sijakosea, haoa ukija na case itaishia kutibiwa kwa dawa labda na mapumziko ya mda ila hawalazi.

Wanafanya procedures ndogo ndogo kama kufunga vidonda.

Kituo cha afya

Kuna medical officer(s) wenye bachelors na COs wanakuwepo,

Hapa huduma za zahanati zinakuwepo plus upasuaji mdogo unaweza kuwepo kama vifaa vipo.

Wanalaza pia.

Hospitali ya tufaa ya wilaya.

Wanaenda zaidi kuna kiwepo na huduma nyingi zaidi, na vifaa vingi zaidi. Kuna weza kuwepo na (ma)daktari bingwa.

Upasuaji mkubwa, wanalaza na specialized servicers kama macho, kinywa, zinakuwepo. Japo hata kituo cha afya zinaweza kiwepo.

Hospitali ya rufaa ya mkoa.


Kunakuwepo na madaktari bigwa wa disciplines mbali mbali, kama wa kina mama, upasuaju, mifupa na kadhalika. Wanakua na vifaa vingi na wafanyakazi wa kutosha kutoq huduma husika wa disciplines mbali mbali kama , phisiotherapy, magonjwa ya akili wanaweza kiwepo nakadhalika.

Specialized referal hospotal (zanol referal)

Hizi zinakua za kanda, mfano. KCMC, BUGANDO, DODOMA, MBEYA.

Hizi zinakua na superspecialities.

Mfano, daktari wa upasuaji wa watoto, mtaalamu wamionzi(Radiologists and Radiographers) wa mifupa na misuli"muscle skeletal"

Etc...

katika levle hii sio ajabu mgonjwa akapewa rufaa kutoka labda bugando akapelekwa kcmc and vice versa. Kutegemeana na utaalamu husika unapatikana wapi.

Mda mwingine hata kutoka muhimbili wakipelekwa kwenye hospitali hizi.


Hospitali ya rufaa ya taifa. MIHIMBILI.

Pia kuna taasisi ambazo zinajitegemea kutokana na specialization na umuhimu wa huduma husika, mfano, MOI, OCEAN ROAD, JAKAYA KIKWETE.

Kwa ufahamu wangu, naweza kuwa sio perfect sana
 
Wagonjwa kutoka hospitali ya rufaa pia huwa referred kwenye DDH yaani hospitali za wilaya. Kama complex issues zimeshatibiwa wanarudishwa kupata muda wa kurecover
Sawa madame
 
Back
Top Bottom