Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 339
- 678
Na Elius Ndabila
0768239284
Kumekuwa na maneno mengi kuelekea uchaguzi wa CHADEMA unaofanyika katikati ya mwezi huu.
Wapo watu wanaotafusiri kitendo cha Mh Mbowe kugombea tena kama ni UDIKTETA. Wanaozungumza hili ni wale wanaojielekeza kwenye tafsiri shambulizi ya demokrasia.
Ninadhani ni muda mwafaka wa kutofautisha hizi zana yaani demokrasia na UDIKTETA.
Ninadhani Waganda na nchi zingine za afrika zilizowahi kuwa chini ya tawala za kidikite wakisikia tunasema Mbowe ni DIKTETA wanashangaa.
Wanashangaa kwa kuwa wao UDIKTETA wameuishi chini ya Idd Amini Dada. Labda niwakumbushe kuwa Demokrasia ni kitendo cha kiongozi kupatikana kwa njia ya kura.
Na mara zote demokrasia inawapa waliowengi na kuwanyima wachache ijapo yapo mazingira yanayopa wachache hasa inapohusishwa kura ya Turufu.
Lakini unaposema mtu ni DIKTETA ni pale huyo mtu anapojitwalia uongozi kwa nguvu na kusimamia kila kitu. Yeye ndiye anaamua muda gani mlale, muongee, mtembea n.k huyu ndiye DIKTETA.
Lakini mtu anayepatikana kwa kura za wengi huwezi kusema ni DIKTETA. Afrika hana kiongozi DIKTETA kwa sasa.
Mtu kukaa muda mrefu madarakani kwa kupigiwa kura si UDIKTETA ni matakwa pia ya demokrasia.
Katiba yao haijatoa ukomo wa kugombea Uwenyekiti. Kama tukisema Mbowe kwa miaka 15 hii ni DIKTETA vipi kwa wabunge wetu waliongoza majimbo yetu kwa zaidi ya miaka 20 nao ni madikteta?
Binafsi ninadhani tunataka kubadili dhana hailisi ya neno DIKITETA. Tunataka kulea kizazi ambacho hakitataka kufikiri bali kushambulia.
Hapa Mh Mbowe akipigiwa kura na kushinda siyo DIKTETA, ninadhani tingetumia msamiti HANA BUSARA. Yaani atumie BUSARA kuwaachia wengine nao waonyeshe mchango wao.
Lakini kwa kusema ni DIKTETA tutakuwa hatukumwelewa Abraham Lincoln Baba wa Demokrasia. Ninadhani tutumie hoja zingine kumpinga Mbowe hoja ya UDIKTETA ni dhaifu.
Mh Sumaye Waziri Mkuu Mstaafu wakati anatangaza kupumzika siasa alikuwa anajaribu ku pre empty dhana hii akitaka kuuminisha umma kuwa hakuna demokrasia.
Sumaye alisahau kuwa hakuna siasa nyepesi. Na kunapokuwa na siasa ngumu hakuhalalishi kuwa ni UDIKTETA.
Hakuna UDIKTETA hapo. Tumetoka kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa wenzetu CUF, CHADEMA, ACT na washirika wao waligoma kuingia kwenye uchaguzi na CCM kushinda.
Hapa huwezi sema CCM madikiteta wakati vyama hivyo vilishiriki hatua zote ila baada ya kuzidiwa mbinu vikijitoa. Hapo theory ya demokrasia ilikuwa applicable.
Mh Mbowe si DIKTETA, bali inahitajika BUSARA ya yeye kuwaachia wengine nao waonyeshe mchango wao.
Lakini kama hatatumia BUSARA na akaendelea kuongoza hata kwa miaka 30 lakini kwa kuuruhusu mchakato wa kuchukua fomu watu na kupigiwa kura hautakuwa ni UDIKTETA bali itakuwa ni DEMOKRASIA inamuweka.