Kuna Tofauti ya Kuwa Peke Yako na Kuwa Mpweke

Kuna Tofauti ya Kuwa Peke Yako na Kuwa Mpweke

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Screenshot_20241201_115253_Google.jpg

Kuna tofauti kubwa ya kuwa peke yako (alone) na mpweke (lonely),lkn kwa bahati mbaya sana mtu ukiwa peke yako unaonekana eti upo mpweke.

Hakuna ubaya kuwa peke yako maadam tu unafurahia kampani yako binafsi ila kama uko peke yako na hujifurahii ukiwa mwenyewe hapo sasa unakuwa mpweke

Lakini upweke unasababishwa na mambo mengi na hii isichukuliwe katika mapenzi tu,bali upweke upo hata nje ya mapenzi na mara nyingi watu ambao wana roho mbaya na roho ya kwanini huwa wapweke sana

Unajua kwanini? Kwasababu kitendo cha kuwafanyia wengine fitina na kuwaharibia maisha yao,au ndoa zao au hata biashara zao,mwisho wa siku ukiwa peke yako unapata hisia za majuto na huzuni pia,ukifikiria ndoa zimeparaganyika kwasababu yako,kazi na biashara hivyo hivyo lazima utakuwa na hisia za majuto,na hapo ndio huwa mpweke.

Kinyume chake ukiwa mtu mwenye moyo safi na roho nzuri,unasaidia watu changamoto zao,unaunganisha undugu,unasuluhisha ndoa zinazo kuelekea kuvunjika,ukikaa peke yako kuna hisia nzur unazipata kuona wengine wamefanikiwa kwasababu yako,yatima wamekula na kwenda shule kwa hela zako,ndoa zina furaha kwasababu yako,hakika hauwi mpweke bali utafurahia kila dakika na sekunde za kuwa hai hapa duniani.

Ikiwa uko mpweke halafu ukataka kupoteza upweke wako labda kwa kusoma kitabu,au kucheki movie au kufanya jambo lolote ambalo unadhani litakuondolea upweke,ujue utaondoa upweke kwa mda tu lkn baada ya mambo upweke uko pale pale,ni sawa na mtu mwenye matatizo akinywa pombe zikiisha tu shida zipo pale pale

Kwahiyo dili na sababu ambazo zinakufanya uwe mpweke,badilisha maisha yako,kuwa na roho safi na moyo safi hakika hautakuwa mpweke ila utakuwa peke yako ambaye unafuraha na amani tele

Kuwa peke yako sio shida ila shida ni kuwa mpweke


Ni hayo tu!
 
Nilijifunza hii kwa the late dr. Myles Munroe.
Nikaelewa kua kuna walio na kampani za watu lakini wako na upweke (loneliness) na kuna walio pekeyao(alone) lakini hawana loneliness
 
Nilijifunza hii kwa the late dr. Myles Munroe.
Nikaelewa kua kuna walio na kampani za watu lakini wako na upweke (loneliness) na kuna walio pekeyao(alone) lakini hawana loneliness
Ni sahihi kabisa,mfano kuna watu wapo kwenye ndoa lkn ni wapweke sana hakuna ukaribu (bond) kati yao,hakuna connection kati yao hao wapo kama house mate tu walioamua kuishi nyumba moja
 
Back
Top Bottom