Ngoja namimi "nikubabaishe" kwa kadri ya uelewa wangu.
Kuna maneno mawili ya lugha ya kiingereza yanayotumika kuelezea eneo ambalo bahari inapakana na ardhi. Maneno hayo ni shore na coast.
Kwenye shore tutapata neno ufukwe, kwenye coast tutapata neno pwani, makinika nami katika udadavuzi wa maneno hayo.
Kama maneno yote yanamaanisha mpaka wa bahari na ardhi je, nini tofauti yao....?
Coast yaani Pwani imeenda mbali zaidi ya kuelezea mpaka wa bahari na ardhi pekee, bali inajumuisha eneo kubwa zaidi lenye uoto, hali ya hewa na tabia ya nchi inayofanana na lile eneo ambalo bahari inapaka na ardhi. Na ndio maana tunakua na eneo kubwa mbali kutoka maji yalipoishia tunalitambua kama ni eneo la Pwani, mfano hapa ni kwamba hadi kibaha kule sehemu ya Pwani ya bahari ya Hindi.
Kwa upande mwingine, shore ni mpaka wa bahari na nchi kavu ila hapa tunazingatia zaidi lile eneo ambalo ni makutano haswa ya maji na ardhi. Kuna aina kuu tatu za shore,
1. Rocky shore (hii ina miamba)
2. Muddy shore (ni ya tope)
3. Sandy shore (hii ni ya mchanga).
Sandy shore ndio imepewa jina BEACH kwa kiingereza, ambapo kwa tafsiri ya kiswahili tunaita UFUKWE.
Nadhani utakua umenielewa nikiishia hapo kwa upande wa shore. (Maana hapo kwenye aina kuna vitu kibao sijaeleza nikiamini kwamba lengo ilikua tu kufahamu ufukwe ni kitu gani).
MWAMBAO:
Hapa mkuu sina uelewa mzuri juu yake lakini kwa fikra zangu tu, ninafikiri kwamba neno mwambao linatumika zaidi kuelezea masuala mbalimbali yanayohusiana na Pwani na wakazi wake. Mfano ni tamaduni za jamii zinazopatikana maeneo ya Pwani kama vile muziki wa mwambao kama alivyoeleza mdau hapo juu, mapenzi ya kimwambao n.k.
Na kwa kumalizia tu, neno mwambao lina ukaribu sana kimaana na neno "pembezoni mwa ....." kwahiyo maana yake kwa muktadha huu itakua imejiweka mahala fulani baina ya neno Coast na Shore.
Huo ndio mwisho wa ubabaishaji wangu.