Kuna ubaya wanawake kutoa treat kwa wapenzi wao na ikajulikana hivyo?

Kuna ubaya wanawake kutoa treat kwa wapenzi wao na ikajulikana hivyo?

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Siku mwanaume huna pesa, then mpenzi/mke wako kaamua mtoke out kwa treat yake(anagharamia yeye hiyo outing).

Muda mfupi kabda ya bill kuletwa anafungua pochi anafumbata kitita cha noti kadhaa kiganjani mwake kisha kwa siri/kificho anakupatia ili ufanye malipo mtakapoletewa ankara ya huduma mliyopatiwa

Hua najiuliza kwani wanawake hujihisi vipi wakilipa wao moja kwa moja? Au wanahisi wanaume tunajisikia vibaya kulipiwa bill na wapenzi wetu?

Hii ni tofauti kama utatoka out na dada yako. Kama ameamua iwe ni treat yake basi atalipa yeye moja kwa moja. Ila na yeye akimtoa out mwanaume wake atampasia pesa ili mwanaume ndio alipe!!!😀😀😀

ANGALIZO: Huu ni uzoefu wangu kwa wanawake watatu au wanne tu na wala sijafanya utafuti kujua ukubwa wa jambo hili
 
Kiafrika mwanamke ni kiongozi,hivyo anakupa heshima yako ya ukuu na wala si vinginevyo...!!!
Asili ya mwanamme ni kuongoza na kibongobongo akilipa mdada mhudumu anaweza anza kukuonesha dharau ujue..tunajuana siye
Nadhani ni kautamaduni kazuri haka raymage acha tu kaendelee😀😀😀
 
Kukazia tu mwanamke anayefanya hivyo ujue she is a keeper aisee!

Mpende na umuheshimu.

Back to the topic mimi naona ni ile kutaka kututunzia heshima kama wanaume tu coz we're naturally meant to be the providers and not the other way round. [emoji3]

[emoji3577]
 
Naaaam sheikh.....
Kwahiyo ukimpata huyo anaekulipia bill umeokota dhahabu ila ndio kazidiwa hadi na kuku ujue 😁
Evelyn,

Hiyo inatakiwa iwe mara chachechache na sio mara zote. Kiuhalisia na kiasilia kweli kulipa bills ni jukumu la mwanaume, mengine ni bonus tu😀😀😀
 
Back
Top Bottom