Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Na Lula wa Ndali Mwananzela (Raia Mwema)
President Kikwete and King Mswati III at a SADC meeting in Swaziland. Photo/FILE
SAUTI zao zinazidi kupaa na mlio wake unazidi kuitikiwa katika kona mbalimbali za taifa letu. Mwangwi wa hoja zao unazidi kunguruma kwa uchokozi kama upepo unaotangulia kimbunga.
Tunaambiwa mambo mawili ambayo yanaletwa kwetu kama ukweli: Kikwete ndiye mgombea pekee anayefaa kusimamishwa na CCM; kwani hakuna mwingine na pili; ndiye mgombea anayekubalika zaidi; kwani hata alipoingia madarakani ni asilimia 80 ya wapiga kura waliomchagua. Haya tunaambiwa ni ya kweli na kwa kipimo cha haraka haraka tunawapa jibu; "tumekubali".
Kutokana na hayo mawili, sauti hizo zimeamua kupendekeza hitimisho lifuatalo: Rais Jakaya Mrisho Kikwete awe mtu pekee kuchukua fomu za kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Sauti nyingine zimeanza nazo zinataka kwenda mbele zaidi na hizi zipo kwenye upinzani.
Hizi zinataka Rais Kikwete awe mgombea pekee wa urais mwaka huu. Wote hawa wanasema hayo kwa sababu hizo mbili: Kwamba Kikwete anakubalika zaidi na kuwa hakuna mtu mwingine anayeweza kuwa mbadala wake iwe ndani ya CCM au nje yake!
Tuliyaona haya pia wakati Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alipokuwa akikaribia kumaliza kipindi chake cha kwanza cha urais. Walijitokeza watu (tena baadhi yao wazito) na kupendekeza kwamba kusiwe na wakujitokeza CCM kuchuana naye atakapochukua fomu kuwania urais kwa kipindi cha mwisho cha miaka mitano.
Sasa jambo hili limerejea tena kwa kishindo katika utawala huu wa sasa wa awamu ya nne chini ya Rais Kikwete, na ndiyo maana katika makala hii nina pendekezo. Napendekeza wale watetezi wa dhana ya "ugombea pekee" wasiishie hapo; bali waende mbele zaidi.
Kama kweli wanapenda na kweli wanataka wawe chini ya uongozi wa rais kwa muda mrefu zaidi bila kujali uchapakazi wake, basi, wasiishie kupigia debe dhana ya "mgombea pekee". Waende mbele na kufikia kwenye hitimisho la kimantiki, kwamba Tanzania tuanzishe mfumo wa utawala wa kifalme!
Sasa sisemi jambo hili kimzaha; kama mtu anavyoweza kufikiria. Nimepima faida ya kufanya hivyo kwa taifa na kwa siasa za nchi yetu. Nimeona kuwa wananchi wote tukikubaliana na hoja zao hatuna budi kufikia hitimisho hili kuwa Tanzania inafaa kuwa na utawala wa kifalme.
Unaweza kushangaa kuna faida gani kuwa na utawala wa kifalme?
Kwanza, tukiwa na mtawala mmoja ambaye ni Mfalme hatutalazimika kufanya chaguzi za rais kila baada ya miaka mitano! Kwa vile tunakubaliana na dhana ya ‘mgombea pekee' na hatutaki mtu mwingine yoyote awe CCM au nje yake ajitokeze kugombea, basi, ni wazi mfumo wa kifalme ndiyo unaotufaa na unaotustahili.
Kwa hiyo, tutaokoa fedha nyingi sana (mabilioni) ambazo hutumika kwenye uchaguzi. Fedha hizo zingetumika katika kuchukua fomu, kuzunguka kupata wafadhili, kampeni na baadaye uchaguzi. Kiasi hicho kinaweza kutumika kwenye shughuli nyingine za kuwaletea wananchi maendeleo.
Pili, tukiwa na mfalme; hatakuwa na sababu ya kufanya mambo kwa ajili ya kuwaridhisha watu wake waliomkampenia kwa sababu hakutakuwa na uchaguzi. Hivyo, Mfalme atakuwa anatilia tu mkazo kufanya mambo yenye maslahi ya Taifa.
Fikiria kwamba marais wetu wote ilibidi mara kwa mara wawaeleze wananchi mambo waliyoyafanya ili wasije kutoswa kwenye uchaguzi. Sasa tukiwa na mfalme wa kudumu, yeye hatokuwa na wasiwasi wa kutuelezea wananchi au kutubembeleza bembeleza. Atakuwa ni mtawala wetu kweli kweli; kwani hatokuwa na hofu ya kupoteza kura au kupingwa sijui na mpinzani gani!
Nne, mfumo huu utavisaidia vyama vya upinzani vile vile. Mara kwa mara wapinzani wanatumia muda mwingi ili wafikirie jinsi ya kugombea nafasi ya urais wakati tayari wanajua watashindwa hata kabla upigaji kura wenyewe haujafanyika!
Hili limekuwa likisababisha migogoro ya mara kwa mara ndani ya vyama hivyo, na kila unapokaribia uchaguzi mkuu, basi, kunakuwa na mvutano wa hapa na pale. Kwa kuwa na mfalme wa kudumu, hata viongozi wa upinzani watakuwa hawana sababu ya kugombania nafasi ya uenyekiti ili waje kugombea urais wa nchi.!
Kwa hiyo, wapinzani watatilia mkazo zaidi viti vya ubunge kuliko urais; kwani tayari mtawala (mfalme) tunaye anayekubalika na wananchi wengi, kupendwa na kuheshimiwa na vizazi vingi vya Watanzania!
Tano, itakisaidia pia Chama Cha Mapinduzi (CCM); kwani kwa mara ya kwanza tutaondoa masuala ya mizengwe ndani ya Chama. Tukiwa na mfalme wa kudumu, wana CCM hawatakuwa na sababu ya kuharibiana majina, kuchafuana (hata ikibidi kufoji picha) au kuitana majina mabaya.
Hii itakifanya Chama Cha Mapinduzi kurudi kama wakati wa Mwalimu Nyerere ambapo walijua kabisa mgombea wao ni mmoja tu na uchaguzi wa ubunge ndio ulikuwa una utamu wake.
Sasa hizo ni faida chache tu. Nina uhakika kama taifa na wasomi wetu wakifikiria sana wanaweza kuona faida nyingine nyingi zaidi kuliko hizo, na watakubaliana na mimi kuwa tukimpata mfalme mzuri anayekubalika na wengi (chaguo la Mungu) kutaliinua taifa letu mbele ya macho ya wafadhili na kutuonesha ni jinsi gani ‘tumekomaa' kidemokrasia.
Najua kwa haraka pingamizi kubwa kwenye hoja yangu hii linaweza kutolewa; kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na tuna vikomo vya uongozi, na hivyo ni lazima viheshimiwe.
Watasema kwamba Tanzania inao watu wengi wanaofaa na CCM inao watu wengi wanaofaa na kwamba marais wetu wataheshimu Katiba na kung'atuka baada ya vipindi vyao kukoma.
Jibu langu kwao ni kwamba kama tayari tuna rais anayekubalika zaidi sasa hivi na kupendwa kiasi cha kutaka watu wengine wasigombee urais, basi, tayari demokrasia imeshapoteza maana yake.
Kama kuna watu wenye kuipigia debe dhana ya ‘mgombea pekee' kwa sababu aliyepo sasa (Rais Kikwete) anakubalika, na hivyo kuwataka watu wengine (kwa kutumia haki yao ya kidemokrasia) wasijitokeze kumpinga, basi, mfumo wa kifalme ndiyo unaotustahili; maana demokrasia hatuiwezi!
Haiwezekani iwe demokrasia kwa Kikwete kutogombea kwa sababu ya ukomo, lakini isiwe demokrasia kwa watu wengine kumpinga!
Ni kutokana na jibu hilo naamini tunaweza kwenda mbele zaidi na kufikiria kuwa na utawala wa kifalme kama zilivyo baadhi ya nchi duniani.
Napendekeza badala ya kupoteza fedha kuandaa Uchaguzi wa Rais, uanzishwe mchakato wa kushawishi umma kuukubali mfumo wa kifalme ili baadaye atafutwe mtu anayefaa, atangazwe kuwa ni Mfalme na familia yake iwe Familia ya Kifalme (Royal Family).
Sasa najua unaweza ukacheka pendekezo langu hilo ukidhania natania.
Huko mbeleni naweza kupendekeza jinsi gani tunaweza kumpa maisha anayostahili Mfalme (sijui kama tufuate mfano wa yule wa Swaziland, Mswati (III). Tukiwa na Mfalme na sisi tutakuwa tumejiweka kwenye mataifa ambayo yana wafalme na yameendelea au yanapiga hatua mbele ya maendeleo kama UAE au kule Jordan.
Hivyo, uchaguzi huu wa 2010 uwe wa wabunge na kura ya maoni juu ya kubadilisha mfumo wetu wa kijamhuri ili tuwe taifa linaloongozwa na mfalme! Sijui wenzangu mnaonaje?