DOKEZO Responded Kuna uchakachuaji wa ujazo wa mitungi ya Gesi kwa baadhi ya Kampuni; Wananchi tunaumia

DOKEZO Responded Kuna uchakachuaji wa ujazo wa mitungi ya Gesi kwa baadhi ya Kampuni; Wananchi tunaumia

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Kwa nyakati tofauti Serikali na wadau mbalimbali wamesikika majukwaani wakihamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kulinda mazingira, kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kuokoa maisha ya maelfu ya watu, hata hivyo kwenye jamii kumekuwa na wimbi la malalamiko kuhusu uchakachuaji wa ujazo wa mitungi ya gesi. Hali hii inatokea wakati ambapo wananchi pia wamekuwa wakilalamikia kupanda kwa bei ya gesi ya majumbani, ambayo kwa wengi haiendani na hali halisi ya maisha yao.

Soma: WMA: Wananchi wana haki ya kujiridhisha gesi wanayonunua ina uzito sahihi, wauzaji wawe na mizani

Kwa takribani miaka 10 nimekuwa nikitumia gesi ya kampuni X yenye ujazo wa kilo 15. Kwa kipindi chote hicho, nilikuwa nikijaza mtungi na gesi ikadumu kwa muda mrefu kulingana na matumizi yangu. Hata hivyo, mara mbili za mwisho nilipojaza mwaka huu, nimeshangazwa na jinsi gesi ilivyoisha kwa haraka, licha ya kwamba matumizi yangu yamepungua ikilinganishwa na zamani ambapo nilikuwa napika mara kwa mara.

Mara ya kwanza gesi ilipoisha mapema, nilimpigia simu wakala ambaye huniletea mtungi huo na kumweleza changamoto hiyo. Alinijibu kwamba huenda nilikuwa nimeufunga vibaya, hivyo gesi ikawa inavuja. Sikubishana naye sana, ingawa sikuwahi kuona dalili zozote za gesi kuvuja. Kwa kawaida huwa mwangalifu sana katika kuhakikisha usalama wa matumizi ya gesi kutokana na hatari zinazoweza kujitokeza.

Baada ya tukio hilo, nilijipa muda na kuamua kulifuatilia kwa karibu. Wakati huo huo, jirani yangu ambaye hutumia gesi ya kampuni Z naye alikuwa akilalamikia jambo hilo hilo, akisema gesi yake imeisha mapema tofauti na alivyozoea. Nilipojaza mtungi mwingine, niliongeza umakini zaidi katika kuufunga na kuhakikisha hakuna uvujaji wowote. Hata hivyo, gesi hiyo nayo iliisha kwa muda mfupi, ilhali matumizi yangu yalikuwa madogo zaidi kuliko zamani ambapo nilikuwa napika mara nyingi na kwa muda mrefu.

Nilimtafuta tena muuzaji na kumweleza kuwa tatizo limejirudia. Alinieleza kuwa si mimi pekee ninayelalamika, kwani wamekuwa wakipokea malalamiko ya aina hiyo kutoka kwa wateja mbalimbali. Hata hivyo, alisema changamoto hiyo inaonekana kuwa upande wa wazalishaji au mawakala wakuu, kwa kuwa wao ni wasambazaji tu wanaonunua na kuuza bidhaa hizo.

Nimeamua kuibua hoja hii kwa sababu hata ofisini ninakofanyia kazi, wenzangu wengi wamekuwa wakilalamikia changamoto kama hiyo. Aidha, nilipozungumza na baadhi ya wasambazaji wa gesi waliopo mtaani, walidai kuwa siku hizi malalamiko yameongezeka na kwamba wamekuwa wakiyawasilisha kwa kampuni husika zinazotuhumiwa.

Ni kweli kwamba wananchi wengi hawana utamaduni wa kupima uzito au ujazo wa mitungi ya gesi kabla ya kuinunua. Hata hivyo, hata pale mtu anapotaka kupima, kuna malalamiko kwamba baadhi ya mizani inayotumika siku hizi nayo huchezewa, jambo linalozua mashaka zaidi.

Wito wangu kwa Wakala wa Vipimo (WMA) ni kuongeza usimamizi na ukaguzi wa suala hili. Endapo itabainika kuwa kuna kampuni inayohusika na uchakachuaji wa ujazo wa gesi, ichukuliwe hatua kali za kisheria ili kulinda haki za watumiaji na kurejesha imani ya wananchi.

Hali hii inaumiza wananchi wengi ambao tayari wanajitahidi kununua gesi kwa gharama kubwa, lakini bado wanakabiliwa na madai ya kupunjwa katika ujazo. Mitungi huandikwa kuwa na ujazo wa kilo tano au kilo 15, ilhali baadhi ya watumiaji wanagundua uhalisia kuwa tofauti. Malalamiko kama haya yanaonekana kusikika kutoka kwa watumiaji wa kampuni mbalimbali za gesi zinazotumika nchini.

Iwapo changamoto hizi hazitashughulikiwa kwa haraka, zinaweza kudhoofisha na kuchelewesha jitihada za Serikali na wadau za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, ambazo zimekuwa zikisisitizwa mara kwa mara katika majukwaa mbalimbali. Wananchi tunahitaji uhakika kwamba wa thamani halisi ya fedha tunazolipa na hiyo ni haki yetu inapotokea tofauti tunaumia.

Pia soma ~ Dar: Wachakachuaji wa gesi za majumbani wakamatwa Malamba mawili
 
Mimi ni muhanga wa hilo,gas ninunue apr afu june iishe wakati uko nyuma nilikuwa natumia si chini ya miezi 4 na matumizi ni yaleyale.

Ni kampuni zote sasa hvi ..... Waliniambia nibadilishe regulator ndo npo nafatilia ila nahisi kuna kamchezo.
 
Upo sahihi kabisa mkuu.
Nilishangaa pia kutumia gas (15kgs) kwa mwezi 1 na sina matumizi makubwa.

Ngoja nione awamu hii ( Leo nimekamilisha mwezi 1).

Nilitaka kulisema hapa kabla yako.

MSITUFANYIE HIVYO TAFADHALI.
 
hii mitungi midogo kuna baadhi ya kampuni vifungo vyake tu ni kituko utadhani kimeegeshwa
 
😢
 

Attachments

  • IMG_6347.jpeg
    IMG_6347.jpeg
    208.1 KB · Views: 12
Back
Top Bottom