A
Anonymous
Guest
Kuna changamoto ya ucheleweshaji wa majibu kutoka DAWASA kwa barua za maombi ya ushauri na maoni kuhusu miradi inayofanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA).
Barua tunazowasilisha katika ofisi za DAWASA Mwananyamala huchukua hadi miezi sita bila majibu, licha ya kufuatilia mara kwa mara. Wakati mwingine tunambiwa kuwa majibu yanasubiri kusainiwa na Mkurugenzi.
Hali hii huchelewesha kwa kiasi kikubwa mchakato mzima wa EIA, kwani taasisi hiyo ni miongoni mwa wadau muhimu wanaotakiwa kutoa maoni kuhusu miradi husika.
Tunaomba mamlaka husika kuingilia kati na kuhakikisha mifumo ya utoaji majibu inaboreshwa ili kuepusha ucheleweshaji unaokwaza utekelezaji wa miradi.