Kuna udikiteta Amazonia lakini utapita na watapita

Kuna udikiteta Amazonia lakini utapita na watapita

Magufuli 05

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2023
Posts
1,990
Reaction score
3,824
Hakuna kitu Cha milele

Dunia tunapita kitabaki milele ni milima. Kama imefikia hatua Katika nchi ya Amazonia dini zinafutwa kisa tu zinapinga utekaji na manyanyaso kwa raia basi hii sawa kabisa au zaidi hata ya enzi za mkoloni.

Wakati dini na makanisa zilipokuwa zinasifu hazikuwahi kuambiwa zinachanganya siasa na dini. Baada tu ya kuhoji kuhusu nani anayeteka watu, Dini zimeanza kufungiwa. Kwahiyo kuteka watu ni siasa kumbe.

Wapo wajinga wanashangilia. Lakini hawajui kama wanashangilia anguko la wajomba zao.

Dini inahubiri usawa,haki na ustawi. Dini inahuruma,dini inaunganisha. Kwanini Leo tunafungia dini?
Kwanini Huwa mnawaita maaskofu na masheikh kwenye mikutano ya siasa kuomba? Hamuoni kama mnachanganya dini na siasa?

Kitendo hiki kitawavua nguo na aibu itakuwa nanyi. Ninavyojua kwa upofu na kiburi Cha mwanadamu hamtaona haya Leo ni kawaida tu kwasababu ya interest zenu lakini muda unakuja mtalia na kusaga meno. Amazonia ni nchi yetu.

Babu zetu waliwinda katika nchi hii na tutawinda katika nchi hii. Dikiteta ataondoka kwa aibu kama alivyoondoka Idd Amini na Mobutu, Bokasa na Samuel doe.
 
Back
Top Bottom